Header AD

header ads

SERIKALI KUPITIA MWONGOZO WA MICHANGO SHULENI




Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa ameongea na Kamishna wa Elimu apitie mwongozo wa michango  shuleni huku akisisitiza kuwa michango ni hiari na mtoto yeyote asirudishwe nyumbani kwaajili ya kutotoa michango.

Prof.Mkenda ameyasema hayo leo Julai 29,2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika mkutano maalumu wa kikazi kati ya Wizara ya Elimu na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.


Pia Waziri Mkenda amesema kuwa Wanafunzi watakaofanya vizuri katika masomo ya sayansi watasomeshwa bure kupitia mpango  'Samia Scholarship' hadi elimu ya juu katika fani za sayansi, uhandisi na elimu tiba.

Katika hatua nyingine Prof.Adolf Mkenda amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kwa dhati kuwekeza katika sekta ya elimu nchini ili iweze kutoa matokeo bora kwa Watanzania na mipango mbalimbali ya Serikali.


"Nchi haziendelei kwa sababu ya rasilimali zake, bali kuwekeza katika elimu, "Nchi haziendelei kwa sababu ya rasilimali zake, bali kuwekeza katika elimu. Hivyo tunaendelea kufanya maboresho makubwa ili kuhakikisha tunafikia dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu ya kuwekeza katika ubora wa elimu na upatikanaji wake.Na katika ubora utahakisi mahitaji katika maeneo husika,"amesema Prof.Mkenda.
SERIKALI KUPITIA MWONGOZO WA MICHANGO SHULENI SERIKALI KUPITIA MWONGOZO WA MICHANGO SHULENI Reviewed by Fahadi Msuya on July 29, 2022 Rating: 5