Header AD

header ads

MILANGO IPO WAZI UWEKEZAJI KWENYE SEKTA MISITU.




Wadau wa ndani na nje ya nchi wamehamasishwa kuwekeza kwenye Sekta ya  Misitu kwa kuwa sekta hiyo inakuwa kwa kasi kutokana na mahitaji yake kuwa makubwa kwa jamii.

 Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt Pindi Chana ametoa hamasa hiyo wilayani Mufindi alipotembelea kiwanda cha kutibu Mazao ya Misitu cha  Green Resources  Sao Hill  ambapo amesisitiza  kuwa milango ipo wazi kwa yeyote aliye tayari.

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira mazuri na salama kwa wawekezaji hivyo ni wakati wa wadau  kuchangamkia fursa mbalimbali zilizo katika sekta ya Misitu.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Kiwanda hicho  Bw. John Rabie ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuiimarisha Sekta ya Misitu hali inayochangia upatikanaji wa malighafi ya kiwanda  hicho kwa uhakika na haraka.


Akiwa katika kiwanda hicho cha Sao Hill, Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana ameshuhudia namna mazao ya misitu yanavyokaushwa na kuwekewa dawa kwa ubora.

 Mhe. Balozi Dkt. Chana ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kazi nzuri akiahidi Wizara anayoiongoza itaendelea kutoa ushirikiano unahitajika.
MILANGO IPO WAZI UWEKEZAJI KWENYE SEKTA MISITU. MILANGO IPO WAZI UWEKEZAJI KWENYE SEKTA MISITU. Reviewed by Fahadi Msuya on August 01, 2022 Rating: 5