Header AD

header ads

SERIKALI IMESIKIA KILIO CHA WANA MBEYA: DKT MPANGO



OR - TAMISEMI


MAKAMU wa Rais, Dkt. Philip Mpango ameiagiza Ofisi ya Rais-TAMISEMI kupitia Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kutafuta fedha za kujenga barabara inayotoka barabara kuu kwenda uwanja wa ndege wa zamani.


Dkt. Mpango ametoa agizo hilo leo wakati wa kufungua maonesho ya Wakulima Kitaifa Nane Nane yanayofanyika kwenye Uwanja John Mwakangale jijini Mbeya.


" Serikali imesikia kilio cha wananchi wa Mbeya Mjini kupitia kwa Mbunge wenu makini Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu barabara inayotoka barabara kuu kwenda uwanja wa ndege wa zamani ambako kwa sasa ni vumbi na wakati wa mvua nitope nzito."


" Napenda kuwajulisha kwamba barabara itajengwa kwa lami ili kuwezesha wanachi kufika eneo jipya la wafanyabiashara ndogo ndogo kwa urahisi zaidi.



Dkt.  Mpango amepongeza na naielekeza Ofisi ya Rais-TAMISEMI kupitia TARURA watafute fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo na ujenzi uanze mara moja.

SERIKALI IMESIKIA KILIO CHA WANA MBEYA: DKT MPANGO SERIKALI IMESIKIA KILIO CHA WANA MBEYA: DKT MPANGO Reviewed by Fahadi Msuya on August 02, 2022 Rating: 5