Sheria za Habari kikwazo katika habari za uchunguzi
Na Yusuph Digossi
Imeelezwa kuwa kuwepo kwa sheria za habari zinazoumiza tasnia ya habari kumesababisha kushuka kwa habari za uchunguzi huku ikiripotiwa kwamba baadhi ya wanahabari wamepoteza vifaa vyao kutokana na polisi kuvitwaa kwaajili ya uchunguzi.
Hayo yameelzwa na Wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) alipokua akizungumza kwenye mahojiano ya kipindi cha “Morning Trumpet” kinachorushwa na Televisheni ya Azam Tv Leo Agosti 2,2022.
Marenga amesema kuwa Kwa sasa vyombo vya habari vinaandika kwa uhuru, vinakosoa lakini kilichopo, kama mwandishi ama chombo cha habari kinawindwa, sheria hizi hizi zinatumika kuumiza chombo ama mwandishi.
Ameongeza kuwa Sheria hii imewapa mamlaka makubwa polisi, wanapoamua kukufuatilia na hata kuchukua vifaa vya Mwandishi wa habari , wanaweza kufanya hivyo kwa sheria hii.
Akitolea mfano bora Kwa nchi nyingine Marenga amesema nchi ya Ghana lazima polisi awe na kibali, ndo aweze kufanya hivo lakini kwa hapa Tanzania ni tofauti.
Katika hatua nyingine Marenga amesema, miongoni mwa mambo yanayokwaza tasnia ya habari ni pamoja na sheria kuelekeza usajili wa magazeti kila mwaka.
“kwa magazeti ingetosha kusajiliwa mara moja na sio kila mwaka kama inavyoelekezwa na sheria ya sasa”. amesema Marenga.
Kwa upande wake Wallace Maugo Mhariri wa Gazeti la The Guardian ametoa wito kwa wanahabari kuwa pamoja kufanisha jambo hili marekebisho ya Sheria huku akipongeza uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonesha dhamira ya kweli kuruhusu mchakato wa mabadiliko.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
August 02, 2022
Rating:

Post a Comment