Header AD

header ads

TAASISI YA WOMEN FOR PEACE FEDERATION YAFANYA MAANDAMANO YA AMANI KUHAMASISHA WATU KUSHIRIKI ZOEZI LA SENSA


Baadhi ya wadau na Wanachama wa Taasisi ya Women For Peace Federation wakishiriki maandamano ya amani kwa lengo la kuhamasisha Watanzania kushiriki zoezi la Sensa ya watu na Makazi, maandamano yamefanyika Agosti 03, 2022 Jijini Dar es Salaam

Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda  , Mama Tunu Pinda  akizungumza baada ya kushiriki maandamano ya amani yaliyoandaliwa na taasisi ya Women For Peace Federation kwa lengo la kuhamasisha Watanzania kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi.

Kiongozi wa Kitaifa wa Taasisi ya Women For Peace Federation akizungumza baada ya kushiriki maandamano ya amani yaliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa lengo la kuhamasisha Watanzania kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi


Kiongozi  wa Taasisi ya Women For Peace Federation Mkoa wa Far es Salaam akizungumza baada ya kushiriki maandamano ya amani yaliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa lengo la kuhamasisha Watanzania kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi

PICHA ZOTE NA YUSUPH DIGOSSI- SAUTI ZA MTAA BLOG 

*******************************************

NA YUSUPH DIGOSSI-SAUTI ZA MTAA BLOG

DAR ES SALAAM 

Wanawake  Nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika Agosti 23, mwaka huu ili kuisaidia serikali kupanga mipango ya maendeleo.

Wito huo umetolewa Jijini Dar es Saalam na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda  , Mama Tunu Pinda  ambaye ni mdau wa amani  wakati akizungumza baada ya kushiriki maandamano ya amani yaliyoandaliwa na taasisi ya Women For Peace Federation kwa lengo la kuhamasisha Watanzania kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi.

Amesema kuwa Wanawake  wanayodhamana kubwa kwenye suala hili la sensa kwani wao ndio walezi wa familia  na  wanaotakiwa pia kusaidia kuhamasisha watu wengine kushiriki vyema zoezi hilo.

Ameongeza kuwa Sensa ya mwaka huu itaenda mbali zaidi kwa kutaka kujua idadi ya watu wenye uhitaji maalumu ili Serikali kuwajumuisha katika mipango ya kimaendeleo .

Hata hivyo Mama Tundu Pinda amewakumbusha viongozi wa Dini kuendelea kuwahamasisha waumini kushiriki zoezi hilo .

Katika hatua nyingine Mama Pinda amewataka Wanawake kuendelea kuielekeza jamii haswa watoto kuhusu suala la amani ili kuendana na kauli mbiu ya Women For Peace Federation  na kuishi kwaajili ya wengine.
TAASISI YA WOMEN FOR PEACE FEDERATION YAFANYA MAANDAMANO YA AMANI KUHAMASISHA WATU KUSHIRIKI ZOEZI LA SENSA TAASISI YA WOMEN FOR PEACE FEDERATION YAFANYA MAANDAMANO YA AMANI KUHAMASISHA WATU KUSHIRIKI ZOEZI LA SENSA Reviewed by Fahadi Msuya on August 04, 2022 Rating: 5