TALGWU, PSI WATOA MSAADA WA VITENDEA KAZI KWA WAFANYAKAZI WA DAMPO LA PUGU NA BUGURUNI.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU), Bwana Rashid Mtima akifurahia Jambo na Wafanyakazi wa kukusanya taka Ngumu Dampo la Pugu baada ya kukabidhi vitendea kazi kwa kushirikiana na PSI kwa lengo la kuboresha mazingira ya Wafanyakazi wa kukusanya taka.
Wafanyakazi wa kukusanya taka Ngumu Dampo la Pugu Kinyamwezi wakiendelea na majukumu yao bila kutumia vitendea kazi kitendo ambacho kinaweza kuharatisha afya na usalama wao mahali pa kazi ikiwemo kupata magonjwa ya mlipuko.
Wafanyakazi wa Dampo la Pugu wakiendelea na majukumu yao baada ya kupokea msaada wa vitendea kazi kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kupitia Public Service International PSI'
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU), Bwana Rashid Mtima na Mratibu wa PSI Dr. Everline Aketch wakikabidhi msaada wa vitendea kazi kwa Wafanyakazi wa Dampo la Pugu baada ya kufanya Ziara katika Dampo hilo.
PICHA ZOTE NA YUSUPH MOHAMMED
*****************************************
Na Yusuph Digossi
Dar es Salaam
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kimesema kuwa kinatambua mchango wa wafanayakzi wa kukusanya taka ngumu ambao ni wananchama na wanaotaka kujiunga na TALGWU hivyo chama hicho kimedhamiria kuona namna ya kuboresha mazingira ya watu wanaofanya kazi ya kukusanya taka ngumu.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU), Bwana Rashid Mtima wakati wa ziara katika Dampo la Pugu ambapo waligawa msaada wa vitendea kazi kuptitia Public Service International PSI kwa wafanyakazi wa Dampo hilo ili kuboresha mazingira ya kazi na Afya za wafanyakazi hao.
Akizungumza baada ya kukabidhi vitendea kazi hvyo ikiwemo mavazi maalumu ya kuvaa wakati wa kukusanya taka (overall) na Glovu Mtima amesema kuwa lengo kutoa vifaa hivyo ni kuona kwa namna gani mazingira ya Wafanyakazi wa kukusanya taka Ngumu yanaboreka.
Amesema wanataka kuona katika mfumo mzima wa kukusanya taka ngumu kupitia PSI, wadau wote wanaohusika katika suala la usimamizi wa taka kuona maisha ya mfanyakazi wa kukusanya taka yanaweza yakaboreshwa.
Ameongeza kuwa kazi ya kukusanya taka ina fursa nyingi kwasababu kuna baadhi ya viwanda vinaendeshwa kwa mabaki ya taka ngumu, pia vipop viwanda vinavyozaliosha taka kutoka viwandani na kupeleka dampo pamoja na Serikali kupitia kata na Halmshauri hivyo kuna haja kubwa ya kuboresha mazingira ya wafanyakazi wake.
Katika hatua nyingine Mtima ameeleza kuwa suala la kuboresha mazingira ya wafanyakazi wa kukusanya taka liwe la wadau wote wanaoshiriki katika suala la usimamizi wa taka.
Wakizungumza baada ya kupokea msaada huo baadhi ya wafanyakazi wa Dampo la Pugu wameishukuru TALGWU kupitia PSI kwa kuwapatia vifaa hivyo ambavyo vitarahisisha mazingira ya kufanyia kazi na kulinda afya zao .
Pia wameiomba jamii kuacha tabia ya kuwatenga kutokana na kazi wanayoifanya huku wakisisitiza kuwa kazi hiyo ndio inayowaendeshea maisha yao kijumla.
TALGWU, PSI WATOA MSAADA WA VITENDEA KAZI KWA WAFANYAKAZI WA DAMPO LA PUGU NA BUGURUNI.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
August 06, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
August 06, 2022
Rating:









Post a Comment