Header AD

header ads

WAZIRI BALOZI DKT CHANA KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA, MSUMBIJI



Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt. Pindi Chana leo Agosti 4, 2022  ameshiriki Mkutano wa kwanza wa Kikanda kuhusu Usimamizi Endelevu wa Misitu ya Miombo Jijini Maputo nchini Msumbiji. 

Mkutano huo unahudhuriwa na viongozi wa juu wa Kisekta  kujadili umuhimu ya uhifadhi wa misitu ya miombo huku  msisitizo ukitolewa kwa nchi zote za Afrika kuhakikisha zinaongeza nguvu katika kuhifadhi rasilimali hiyo muhimu  kwa maisha ya Waafrika na Dunia kwa Ujumla.

Katika Mkutano huo wa Kimatifa, Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameambatana na Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo.


WAZIRI BALOZI DKT CHANA KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA, MSUMBIJI WAZIRI BALOZI DKT CHANA KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA, MSUMBIJI Reviewed by Fahadi Msuya on August 04, 2022 Rating: 5