Header AD

header ads

AWESO AWATEUA WATENDAJI WAWILI WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TANGA



Na Hadija Bagasha Tanga, 

Waziri wa maji Jumaa Aweso amewateua watendaji wawili wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Tanga kuwa wakurugenzi wapya wa mamlaka za maji baada ya kufanya vizuri kwenye miradi ya maji na kuwataka kwenda kutoa huduma katika maeneo mengine. 

Waziri Aweso amefanya uteuzi huo wakati wa hafla ya kuaga bodi ya 8 na wakurugenzi wa Tanga Uwasa iliyomaliza muda wake na kukaribisha bodi mpya ya 9 iliyoambatana na ugawaji wa vitendea kazi kwa bodi hiyo. 


Waziri Aweso amesema hatua hiyo ameifanya ikiwa ni sehemu ya kuongeza usimamizi wa miradi ya maji ambayo inatekelezwa katika kipindi cha serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan. 

Walioteuliwa ni Mhandisi Rashid Shaban ambaye alikuwa mkurugenzi wa usambazaji wa maji safi na usafi wa mazingira katika mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga Uwasa na Dora Killo ambaye amekuwa akihudumia kitengo cha huduma kwa mteja katika mamlaka hiyo. 


Waziri Aweso amesema amewateua watendaji hao kuwa wakurugenzi wa mamlaka na kwamba watapangiwa vituo vyao na amefanya hivyo kutokana na kazi kubwa waliyoifanya kwenye kutoa huduma na kusimamia miradi ya maji kwa kuzingatia viwango. 

"Nimefanya maamuzi haya baada ya kuridhishwa na kazi iliyotukuka ambayo imefanywa na watumishi hawa nimefanya hivi wakati ambapo tunahitaji usimamizi thabiti wa miradi ya maji ambayo mheshimiwa Rais Samia ametoa mamilioni ya fedha kwa kuthamini wananchi wake, "alisisitiza Waziri Aweso. 

Akizungumza mara baada ya uteuzi huo 
Mhandisi Rashid Shaban amesema anakwenda kusimamia miradi ya maji na pia amempongeza Mheshimiwa Rais kwa namna ambavyo ameweza kumtumia Jumaa Aweso kwenye Wizara ya maji na kumsaidia kusimamia miradi ya maji Kitaifa kwa maendeleo ya watanzania. 


Mhandisi Rashid Shaban alikuwa Mkurugenzi wa usambazji  maji kwa kipindi cha miaka  12 ambapo mwaka 2018 Bodi iliridhia ateuliwe kuwa meneja Idara ya Ufundi hadi sasa ambayo amekuwa akihudumu hadi sasa. 

Naye Dora Killo amepongeza uamuzi uliofanywa na mheshimiwa Waziri baada ya kuona mchango wao na kwamba hatamuangusha bali ataendelea kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi ya Taifa. 




AWESO AWATEUA WATENDAJI WAWILI WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TANGA AWESO AWATEUA WATENDAJI WAWILI WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TANGA Reviewed by Fahadi Msuya on September 09, 2022 Rating: 5