GF TRUCK YAJA NA MPANGO KUCHANGIA DAMU SALAMA KUPITIA MAONYESHO YA MADINI GEITA
Na Iddy Lugendo
MENEJA Masoko na Mawasiliano kutoka kampuni ya GF Truck Group, Smart Deus amesema kuwa kupitia maonyesho ya tano ya kitaifa ya madini ya mwaka huu 2022 yanayofanyika mkoani geita wamekuja na mpango wa kuchangia damu salama na kutoa zawadi mbalimbali kwa watakaoshiriki kushiriki kutoa damu.
Deus ameyasema haya Septemba 27 mwaka huu katika viwanja vya maonyesho ya madini mkoani humo mara baada ya kutembelewa na mkuu wa wilaya ya geita Wilson Shimo.
Amesema kuwa katika maonyesho ya madini kwa mwaka huu wao kama Gf Truck group na Damu salama watakuwa na huduma ya uchangiaji damu kama sehemu ya mchango wao kwenye jamii.
Amefafanua kuwa katika uchangiaji huo wa damu watatoa zawadi za tisheti lakini kwa upande waendesha piki piki (bodaboda) watatoa vizibao na hiyo yote ni katika kutoa hamasa kwa ajili ya kuchangia damu.
Katika hatua nyingi Meneja Deus amesema kuwa kwa mwaka huu wameingia makubaliano ya kusaidia timu ya mpira wa miguu Geita fc ambayo ni timu inayotoka katika mkoa huo hivyo wanategemea hata wao kushiriki katika zoezi la kuchangia damu.
Pia ameongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na ofa kwa wale watakuja kuna gari au mashine watapewa zawadi mbili moja ikiwa pamoja na kutembelea hoteli yao iliyopo wilayani bagamoyo kwa siku tatu yeye na familia yake na pia zawadi nyingine ni watafanya huu huduma ya matengenezo kwenye mashine ama gari kwa mwaka mzima.
Deus alimaliza kwa kushukuru mkoa na wilaya ya geita kwa ushirikiano wao na hata wadau wadau madini kwa kuendelea kutumia bidhaa zao za Gf truck group.
Kwa upande wa Meneja Mauzo wa Gf Truck Paul Msuku amesema katika kusaidia wachimbaji wadogo mashine walizonazo mteja anaweza kutanguliza kiasi cha malipo na baadae analipa kidogo kidogo mpaka pale atakapomaliza deni.
Amesema kuwa ni nisehemu ya mchango wao katika kumpunguzia mzigo mchimbaji mdogo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo amesema kuwa wanashukuru mchango wa Gf Truck wanaoutoa katika mkoa wa geita huku akiwataka pia kuwekeza pia hoteli maeneo ya fukwe zilipo mkoani humo ikiwemo Nkome na kungineko.
GF TRUCK YAJA NA MPANGO KUCHANGIA DAMU SALAMA KUPITIA MAONYESHO YA MADINI GEITA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 27, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 27, 2022
Rating:





Post a Comment