KANUNI ZA UFUATILIAJI WA MAZAO YA BAHARI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI YATOA NJIA MPYA YA KUSAIDIA UVUVI ENDELEVU WA PWEZA KILWA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Aqua- Farms Organization ( AFO) Jerry Geofrey Mang'ena, Akizungumza katika hafla ya usanifu wa "Kuunda kwa pamoja Mkakati wa Ufuatiliaji wa Kielektroniki wa Uvuvi wa Pweza Kilwa leo Jumatatu Septemba 19 Jijini Dar es salaam
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akiwa katika picha ya pamoja na wadau na wawakilishi wa Taasisi za umma na mashirika ya Kiserikali katika Mkutano wa "Kuunda kwa pamoja Mkakati wa Ufuatiliaji wa Kielektroniki wa Uvuvi wa Pweza Kilwa leo Jumatatu Septemba 19 Jijini Dar es salaam
Wadau na wawakilishi wa Taasisi za umma na mashirika ya Kiserikali wakifuatilia Mkutano wa "Kuunda kwa pamoja Mkakati wa Ufuatiliaji wa Kielektroniki wa Uvuvi wa Pweza Kilwa leo Jumatatu Septemba 19 Jijini Dar es salaam
****************************************************
Na Yusuph Digossi
Waziri wa mifugo na Uvuvi Mashimba Mashauri Ndaki, ameupogeza Umoja wa Ufuatiliaji na Uhalalisho wa Mazao ya bahari (SALT) kwa kufanikisha kutengeza kanuni za Ufuatiliaji wa kielektroniki Kusaidia Uvuvi endelevu wa Pweza Kilwa, ambapo amebainisha kuwa Serikali imetambua umuhimu wa kudumisha uwazi katika mnyororo wa usambazaji wa mazao ya bahari.
Kanuni hizo zilitengenezwa na Umoja wa Ufuatiliaji na Uhalalisho wa mazao ya bahari (SALT) - kwa kushirikiana na wataalam 35 kutoka serikali zinazozalisha mazao ya bahari, mashirika ya uthibitisho, na makampuni ya uzalishaji mazao ya bahari kutoka duniani kote.
Akizungumza katika hafla ya usanifu wa "Kuunda kwa pamoja Mkakati wa Ufuatiliaji wa Kielektroniki wa Uvuvi wa Pweza Kilwa leo Jijini Dar es salaam Waziri Ndaki amesema kuwa Matumizi ya mitandao ya teknolojia inahusika kwenye Ufuatiliaji wa kielektroniki na inauwezo wa kuboresha ufanisi wa utendaji kazi katika sekta ya mifugo na uvuvi ili kuwezesha usambazaji kwa kuandaa taratibu za kuripoti na kufuata utaratibu wa usambazaji wa taarifa.
Waziri Ndaki ameongeza kuwa thamani ya zao la pweza nchini imeongezeka hivyo kutumia Ufuatiliaji wa njia za kielektroniki utasaidia kupata taarifa za kupambana na uvuvi haramu usioripotiwa na usiothibitiwa ambao utasaidia kuongeza kwa pweza.
"Soko la pweza hivi sasa nchini ni kubwa na thamani ya uzalishaji unaongezeka, lazima kuwa na mfumo wa Ufuatiliaji kwa mazao ya vyakula ambao utatusaidia kupambana na uvuvi haramu unaofanyika na hauripotiwi hivyo kupitia mfumo huu wa kielektroniki utatusaidia kupambana nao, lakini pia mfumo huu utasaidia usalama wa chakula kwa watumiaji kwa kuzingatia usimamizi endelevu wa mazingira ya baharini ili tuweze kuvuna pweza salama kwa matumizi ya chakula." Amesema Waziri Ndaki
"Tunaendelea kufungua masoko ya Pweza ili ata wavuvi wadogo kuwawezesha kuuza pweza wao ambao wadau muhimu wanaojihusisha sana na uhifadhi na uvuvi wa pweza ni wanawake. " ameongeza
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Aqua- Farms Organization ( AFO) Jerry Geofrey Mang'ena, amesema kuwa lengo la kualika wadau katika hafla ni kwamba Nchi ya Tanzania inaweza kuwa na Uvuvi endeleve wenye manufaa ya Kiuchumi, Kijamii na Kimazingira ikiwa wadau wote watashirikiana katika kutoa mawazo ya kupanga na kutekeleza Mikakati mbalimbali katika Sekta ya Uvuvi.
Washiriki wa kongamano hilo ambalo wengi wao niwavuvi wameeleza ya kuwa kupita mradi huu wa uzalishaji na uvunaji wa pweza utawasaidia kuongeza kipato chao lakini pia unaenda kufungua fursa kwa vijana wanaohitumi masomo yao kwa ngazi zote za elimu kuweza kutumia elimu zao kujiajiri wenyewe kupitia zao hilo uzalishaji wa Pweza.
KANUNI ZA UFUATILIAJI WA MAZAO YA BAHARI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI YATOA NJIA MPYA YA KUSAIDIA UVUVI ENDELEVU WA PWEZA KILWA.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 19, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 19, 2022
Rating:




Post a Comment