MCHAKATO WA MABADILIKO YA SHERIA YA HAHARI PROF. KITILA AWAPA USHAURI WADAU WA HABARI
Wakati wadau wa habari wakiendelea na mchakato wa kutoa mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya habari ya Mwaka 2016 haswa kwenye vifungu ambavyo vimetajwa kuwa kandamizi aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo ametoa ushauri kwa wadau wa habari kuhusu mapendekezo yaliyotolewa.
Ushauri alioutoa Mkumbo ni kwamba wadau wa habari wanatakiwa kuandaa hoja nzito ambazo zitashawishi na kuchochea mabadiliko ya sheria hiyo .
Akizungumza katika Viwanja vya Bunge ambapo vikao vya Bunge vinaendelea Mkumbo amesema kuwa wadau wa habari wanatakiwa kujipanga watakapofika mbele ya kamati na kutoa hoja zao kwanini baadhi ya vifungu vya sheria hiyo vibadilishwe.
"kwa kawaida wadau wa habari watakutana na kati na kule ndio wanapaswa kueleza hoja zao kwanini wanadhani baadhi ya vifungu hivyo vinapaswa kubadilishwa" amesema Kitila
Ameongeza kuwa kwenye kamati ndio wadau wanapata nafasi ya kutoa hoja zao kwanini wanataka baadhi ya vipengele vifanyiwe marekebisho
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania ( TEF) Deodatus Balile amesema hadi sasa wameona dhamira njema ya Serikali na kama mchakato ukiendelea hivi basi mambo yatakuwa mazuri huko mbeleni.
MCHAKATO WA MABADILIKO YA SHERIA YA HAHARI PROF. KITILA AWAPA USHAURI WADAU WA HABARI
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 23, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 23, 2022
Rating:


Post a Comment