Header AD

header ads

TANTRADE YAWAPIGA MSASA WADAU WA MASOKO MFUMO MPYA WA TAARIFA ZA BIASHARA




MKURUGENZI wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tantrade latifa Mohamed Hamis amewataka wafanyabiashara kutoka kwenye maeneo mbalimbali kutumia mfumo wa Mobile App ili kupata taarifa mbalimbali za biashara.

Amesema kuwa serikali imekuja na mfumo wa taarifa za biashara kupitia simu za kiganjani hivyo,mfumo huo unawataka wadau kutoa maoni yao ambayo yatakusanywa na wataalamu kupitia Mamlaka hiyo ya Maendeleo ya Biashara nchini ili kwa lengo la kuboresha na kuleta tija kwa wadau .

Mkurugenzi Latifa ameyasema haya Septemba 16 mara baada ya kukutana na wadau hao biashara kwa lengo la kuwajengea uwezo na elimu juu ya mfumo huo wa kidigitali ambao utarahisisha wafanyabiashara kupata taarifa za masoko na biashara kwa ujumla.


,,kimsingi Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini Tantrade inakazi nyingi za kufanya japo watu wengi wanajua kazi nikuandaa maonyesho ya sabasaba lakini moja ya kazi zetu ndio kama hizi tunafanya leo kukutana na wadau hawa wa biashara kwa ajili ya kuwajengea uwezo na uelewa juu ya mfumo wa kidigitali utakaotumika kupeana taarifa mbalimbali za kibiashara.amesema 

Nakuongeza kuwa mfumo huu utarahisha mawasilianio kwasababu wadau watakuwa wanapata taarifa mbalimbali kupitia simu zao za kiganjani ,taarifa zitakazohusu bei mbalimbali za mazo ,soko lake,lakini pia kutapungu watu wakati ambao wao wanakaa pale kusubili mkulima aje na mzigo na wao kazi yao nikupandisha bei huku mkulima akisubili kwa muda mrefu.


Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa kabla ya kuja na mfumo wataalam wake kutoka mamlaka hiyo walizunguka nchi nzima kwa lengo la kuzungumza na wadau wakiwampo wakulima na kuandaa taarifa ambayo imekuja na mfumo wa taarifa shirikishi hivyo kupitia kikao hicho cha wwafanyabiashara wanategemea kupata maoni ili kuendelea kuboresha mahala panapohitajika kuboreshwa ili kuleta tija kwa nchi.
 


Kwaupande wake Afisa Biashara wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa serikali imekuja na mpango mzuri na wao kama watendaji kazi yao ni kuhakikisha mfumo huo wa taarifa unaleta tija kwa wadau na unafanya kazi kama ilivyokusudiwa ili kuleta tija.

Naye Katibu wa Soko la Mbagala langi tatu Frank Mapolu Amesema kuwa mfumo huo wa taarifa umekuja kwa wakati muafaka na wao kama wadau wanaipa hongera Serikali kwa kuja mfumo huo ambao kimsingi ukisimamiwa vizuri utaleta manufaa makubwa kwa wadau ambao ni wafanyabiashara.



TANTRADE YAWAPIGA MSASA WADAU WA MASOKO MFUMO MPYA WA TAARIFA ZA BIASHARA TANTRADE YAWAPIGA MSASA WADAU WA MASOKO MFUMO MPYA WA TAARIFA ZA BIASHARA Reviewed by Fahadi Msuya on September 16, 2022 Rating: 5