Header AD

header ads

VITENDO VYA UKATILI VYATAJWA KUWA TISHIO LA MAGONJWA YA AFYA YA AKILI




Na Yusuph Digossi

Watanzania wametakiwa kuungana kwa pamoja kupinga vitendo vya ukatili kwa Wanawake na watoto ambao husabisha kuongezeka kwa magonjwa ya afya ya akili kwa wahanga wa vitendo hivyo

Wito huo umetolewa na   Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi maalumu  Dkt. Nandera Ernest Mhando wakati akifungua Kongamano la Tisa la Kisayansi kuhusu Magonjwa ya Afya ya Akili na Ukatili liloandaliwa na Chuo Cha Sayansi Shirikishi Muhimbili leo Jumatano Septemba 14 Jijini Dar es Salaam.

Dkt Nandera amesema kuwa Asilimia 70 ya Wanawake hufanyiwa vitendo vya ukatili hivyo Jamii inatakiwa kuunga Mkono juhudi za Serikali na wanaharakati kukemea vitendo hivyo.

"Kuzungumzia Changamoto za Ukatili na ugonjwa wa Afya ya  akili ni wajibu wa tafiti na ujumuishi wa wadau mbali mbali”. amesema Dkt Nandera

Awali akimkaribisha DK. Nandera Mhando ili kufungua  kongamano Hilo.  Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi, Muhimbili Prof.Bruno Sunguya amesema lengo la kongamano hilo Ni kukutanisha wadau mbalimbali wa magonjwa ya akili na ukatili nchini ili kupokea matokeo mbalimbali ya Tafiti za Kisayansi na kuyafanyia uchambuzi wa kina.





VITENDO VYA UKATILI VYATAJWA KUWA TISHIO LA MAGONJWA YA AFYA YA AKILI VITENDO VYA UKATILI VYATAJWA KUWA TISHIO LA MAGONJWA YA AFYA YA AKILI Reviewed by Fahadi Msuya on September 14, 2022 Rating: 5