Waziri Mchengerwa aipongeza Yanga Kwa kuendeleza ubingwa ligi ya mabingwa wa Afrika
Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameipongeza Timu ya Yanga kwa kushinda kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga imeshinda mabao 5-0 dhidi ya timu Zalan FC ya Sudani Kusini katika mchezo wa marudiani uliochezwa leo Septemba 17, 2022 kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Amesema watanzania na wanachama wa Yanga wanafurahi kuona wanafanya vizuri katika mashindano haya ambapo amefafanua kuwa Mhe. Rais pia anaipongeza timu hiyo.
Amesema timu hiyo imeonyesha uzalendo ambao unapaswa kuendelezwa ili kuitangaza Tanzania Kimataifa.
Ameitaka timu hiyo kutoridhika na ushindi walioupata leo na badala yake iendelee kufanya mazoezi zaidi ili kujinoa hatimaye timu hiyo iingie fainali na kuweza kurejesha kombe nyumbani.
"Ninatoa wito kwa timu yetu kutobweteka na ushindi tulioupata leo, watanzania wanakiu ya ubingwa wa kombe hili. Tunahitaji kujituma na kutanguliza uzalendo ili tuwape raha watanzania". Amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Yanga imerudiana na Zalan FC leo Septemba 17, 2022 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kama wenyeji wakati Simba itarudiana kesho Septemba 18, 2922 katika Uwanja huu huu wa Mkapa jijini Dar es Salaam katika mashindano hayo hayo na Nyasa Big bullet ya Malawi.
Kapteni wa Timu hiyo Bakari Mwamnyeto amesema huu ni mwanzo wa kutwaa ushindi ambapo amesema timu yake imejizatiti kuchukua kombe hilo
Waziri Mchengerwa aipongeza Yanga Kwa kuendeleza ubingwa ligi ya mabingwa wa Afrika
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 17, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 17, 2022
Rating:




Post a Comment