Waziri Mchengerwa azipongeza Simba na Yanga.
Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa anazipongeza Timu za Simba na Yanga kwa kushinda kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo jioni ya leo Septemba 10, 2022 mara baada ya michezo hiyo kumalizika.
Simba imeshinda mabao 2-0 dhidi ya timu ya Nyasa Big Bullets FC ya Malawi na Yanga imeshinda mabao 4-0 dhidi ya timu Zalan FC ya Sudani Kusini.
Amesema timu hizo zimeonyesha uzalendo ambao unapaswa kuendelezwa ili kuitangaza Tanzania Kimataifa.
Amezitaka timu hizo kutoridhika na ushindi walioupata leo na badala yake ziendelee kufanya mazoezi zaidi ili kujinoa hatimaye timu zote ziingie fainali na kuweza kurejesha kombe nyumbani.
"Ninatoa wito kwa timu zetu kutobweteka na ushindi tulioupata leo, watanzania wanakiu ya ubingwa wa kombe hili. Tunahitaji kujituma na kutanguliza uzalendo ili tuwape raha watanzania". Amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Mabao ya Simba yamefungwa kupitia kwa Moses Photo katika dakika ya 29 na goli la pili dakika ya 83 wakati magoli ya Yanga yalifungwa na Fei Toto dakika 55 na mengine matatu na Fiston Mayele dakika ya 45, 85 na 88.
Yanga watarudiana na Zalan FC Septemba 16, 2022 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kama wenyeji wakati Simba itarudiana Septemba 17 mwaka huu katika Uwanja huo huo wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Waziri Mchengerwa azipongeza Simba na Yanga.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 10, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 10, 2022
Rating:

Post a Comment