Header AD

header ads

Benki ya KCB yaweka rekodi ya kufikia mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni moja kipindi cha robo tatu ya mwaka 2022.



Na Yusuph Digossi - Dar es Salaam

Imeelezwa kuwa Sekta ya Benki nchini imeanza kuimarika tena baada ya kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na Mlipuko wa Ugonjwa wa Uviko 19 huku ikielezwa kuwa biashara nyingi ziliweka mikakati ya kujipanua hasa baada ya athari za Uviko 19 na matunda yake yameanza kuonekana .

Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB  Cosmas Kimario wakati akitoa taarifa ya Benki hiyo kuweka rekodi ya  kufikia mali yenye thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni moja hadi kufikia kipindi cha robo tatu ya mwaka 2022.



"Benki hii imefikia kiwango cha uzani wa mali wa zaidi ya trilioni 1 hivyo beki hii inakua ni miongoni mwao mabenki makubwa zaidi nchini katika utoaji wa huduma kwa wateja wake na hii itatusaidia sisi kama benki kuendelea kuwahudumia vizuri wateja wetu na kwa kiwango cha juu zaidi" amesema Kimario.  

Kimario amesema  mafanikio hayo pia yametokana na mikakati ya Benki kukuza huduma na kuimarika kwa mazingira ya biashara nchini.


Kimario amesema sababu nyingine ya mafanikio hayo ni kuimarika kwa hali ya uchumi nchini Tanzania kutokana na sera nzuri za Serikali ya awamu ya sita na usimamamizi na sera nzuri na benki ya Tanzania.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCB, John Ulanga alisema Benki imeendelea kukua toka mwaka 1997 ilipoanzishwa.


Naye Mkurugenzi wa fedha, wa Benki ya KCB  amesema katika Benki hiyo utoaji wa mikopo umeongezeka kutoka bilioni 330 mwaka 2017 hadi bilioni 623 mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 88.



Benki ya KCB yaweka rekodi ya kufikia mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni moja kipindi cha robo tatu ya mwaka 2022. Benki ya KCB yaweka rekodi ya kufikia  mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni moja  kipindi cha robo tatu ya mwaka 2022. Reviewed by Fahadi Msuya on October 26, 2022 Rating: 5