Header AD

header ads

Kamati ya Bunge yampongeza Rais Samia kwa kuupiga mwingi kwenye Kombe la Dunia, yasisitiza Wizara inaonekana



Na John Mapepele

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imempongeza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake kwenye sekta za michezo ambao umeifanya Tanzania kunga'ra kwenye mashindano ya Kombe la Dunia.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Stanslaus Nyongo ameyasema haya leo Oktoba 25, 2022 baada ya  kupokea taarifa ya Utekelezaji wa  Majukumu ya Chuo cha  Maendeleo ya Michezo Malya iliyowasilishwa kwenye Kamati hiyo na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa



"Waheshimiwa wajumbe wa Kamati sasa kwa hili  naomba Kwa heshima nisimame na kusema kuwa mafanikio haya yote tunayoyapata kwenye mashindano ya Kombe la Dunia ni kutokana na Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwenye michezo" amefafanua Mhe. Nyongo

Amemwomba Waziri Mchengerwa kuzileta timu za Taifa za soka za Serengeti girls na Tembo Warriors kuzileta bungeni ili zipewe pongezi mara baada ya kupambana na kuandika historia ya kuwa timu pekee kufika katika robo fainali za mashindano ya Kombe la Dunia. 

Aidha ameipongeza uongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuwa wabunifu ambapo amefafanua kwamba Wizara kwa sasa imekuwa inaonekana ukifanya vizuri kuliko awali


Akiwasilisha taarifa hiyo  Waziri Mchengerwa amesema Chuo cha Michezo cha Malya kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinakwenda kufanya utafiti kuhusu mchango wa michezo kwenye maendeleo ya uchumi nchini ili kuweza  kuishauri Serikali namna bora  ya kuifanya michezo ichangie kikamilifu kwenye uchumi wa
nchi.


Amesema katika hatua ya kuimarisha michezo nchini, Serikali ya awamu ya Sita inayoongongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samaia Suluhu Hassan inatekeleza miradi mbalimbali katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya ikiwemo ujenzi wa Hosteli yenye ghorofa nne, ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Kukuzia  na kuendeleza vipaji vya michezo na uchimbaji wa kisima cha kisasa cha maji.

Aidha, amesema tayari Wizara imevielekeza vilabu vyote  vya michezo kuwasilisha mipango ya  kujenga  viwanja  kulingana na Sera ya Michezo ambapo amesema  alitoa  miezi sita  ambapo amefafanua imebaki  miezi mitatu.

Amesema dhamira ya sasa ya Serikali ni kukarabati viwanja 5 vya Mwanza, Dodoma, Tanga, Arusha na Mbeya ambapo gharama yake ni takribani  bilioni 70 ili  Tanzania ifuzu  vigezo vya  kuandaa mashindano ya AFCON 2027.

Amesema, Wizara inaendelea kuweka mikakati mbalimbali  ya kutafuta fedha kutoka kila sehemu ili kuweza kufanya  ukarabati wa miundombinu  kutokana na ufinyu wa Bajeti.

Akitolea mfano amesema bajeti kwa ajili ujenzi kwa wa miundombinu yote ya Chuo cha Michezo cha Malya ni Bilioni 52 ambapo amesema hadi sasa tayari Serikali imeshatoa zaidi ya milioni mia tano. 




Wabunge wameomba kuanzisha tawi la chuo cha Malya upande wa Zanzibar ambapo Mhe. Mchengerwa amekubali kulifanyia  kazi.
Kamati ya Bunge yampongeza Rais Samia kwa kuupiga mwingi kwenye Kombe la Dunia, yasisitiza Wizara inaonekana Kamati ya Bunge yampongeza Rais Samia kwa kuupiga mwingi kwenye Kombe la Dunia, yasisitiza Wizara inaonekana Reviewed by Fahadi Msuya on October 25, 2022 Rating: 5