MAMLAKA ZA AJIRA ZAAGIZWA KUENDELEA KULIPA WATUMISHI STAHIKI ZAO KISHERIA
Na Hadija Bagasha Tanga,
Serikali imeziagiza Mamlaka za ajira kote nchini kuhakikisha kuwa zinaendelea kulipa stahiki za kisheria kwa watumishi wa Umma ikiwemo likizo, mafunzo na posho mbalimbali ikiwemo posho ya kuhudhuria michezo kwenye nyanja ya Kitaifa.
Pia Waziri Muhagama amesema serikali inendela kushughulikia changamoto mbalimbali za wafanyakazi ikiwemo malimbikizo ya mishahara ,kupanda madaraja pamoja na ajira mpya ambapo amewataka waajiri nchini kote kuzingatia kuwapandisha madaraja wafanyakazi na kulifanyia kazi swala la ubadilishaji kada ili kuimarisha ufanisi .
Lakini pia amewataka waajiri wote wahakikishe wanafuatilia kwa karibu mienendo ya Watumishi wa Umma nchini na utaratibu mzuri wa kuhakikisha kila mtumishi anapanda daraja bila kucheleweshwa na kuhakikisha upandishaji madaraja hauna upendeleo wa aina yeyote.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama wakati akifungua rasmi mashindano yanayohusisha Watumishi wa Umma kutoka wizara idara na taasisi zote za serikali Tanzania (SHIMIWI) yanayofanyika Kitaifa Mkoani Tanga.
Waziri Mhagama amesema wizara inaendelea kusimamia maagizo ya serikali ya kuhakikisha kuwa Watumishi wote wenye sifa za kupandishwa madaraja yanatekelezwa.
"Niwaambie ndugu zangu katika mambo ambayo Raisi anaendelea kusimamia moja wapo ni kuhakikisha kwamba serikali inaendelea kusimamia haki na stahiki za Watumishi wa Umma katika sekta zote inatekelezwa kwa vitendo"alisema Waziri Mhagama.
"Niwatake waajiri kote nchini kuhakikisha Mamalaka za ajira katika utumishi wa Umma wahakikishe wanatenga bajeti ya kutosha kila mwaka katika mafungu yao , kulipa stahiki za kisheria ikiwemo likizo mafunzo na posho ikiwemo posho ya kuhudhuria michezo katika nyanja ya kitaifa posho hizo zitengwe kwa sababu ni haki ya Watumishi wa Umma kushiriki michezo"
Aidha Mhagama anaendelea kuwataka waajiri kote nchini kuhakikisha wanawapandisha madaraja Watumishi wote wenye sifa na kulipwa stahiki zao hii ikienda sambamba na ufwatiliaji wa mienendo ya utendaji kazi wa wafanyakazi wote .
Akizungumza katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa serikali na afya Tanzania (TUGHE) na katibu mkuu wa shirikisho la wafanyakazi (TUCTA) Henry Mkunda amesema kuwa jukumu lao ni kuwajengea Uwezo wafanya kazi kwa mafunzo mbalimbali ili kuwa kujenga tabia ya kuwekeza hususan kwenye kilimo kabla ya kustaafu.
Aidha Mkunda alisema kuwa vyama hivyo vinaendelea kuwajengea uwezo Watumishi kote nchini mara baada ya kustaafu waweze
Mkunda amesema kuwa wanafanya mafunzo ya wafanyakazi kuhusu kujiandaa kustaafu kwani wanataka wafanyakazi wasisubiri chama cha wafanyakazi kiendelee kuwafundisha mambo mbalimbali yanayohusu haki zao katika sehemu za kazi wameona ni vyema wawaandae wafanyakazi kujua wataishije hata watakapostaafu.
Awali akizungumza mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba amewataka watumishi wote nchini kudumisha uzalendo uwajibikaji, maadili, nidhamu na kujitoa kwa maslahi mapana ya Taifa.
"Nimpongeza Sana Raisi kwa kuendelea kuwekeza kwenye rasilimali watu Kuna changamoto ya Watumishi tuko wengi lakini maadili ya Utumishi wa Umma yanaendelea kuporomoka siku hadi siku nidhamu , uzalendo kujitoa kwaajili ya taifa letu niwaombe sana Watumishi wote kuwa wazalendo kwa maslahi mapana ya Taifa letu" alisema Mgumba.
Awali akizungumza afisa masoko kutoka kampuni ya Agricom Africa ambao ni wadhamini wakubwa wa mashindano ya (SHIMIWI) kwa mwaka 2022 Baraka Konkara kwa kutambua umuhimu wa michezo kwa kila mtu kuweza kupambana na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza wanaungana na serikali katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
"Kampuni hiyo ilizindua kampeni ya mtumishi shambani ambayo umejikita katika kuwainua wakulima kwa kuwawezesha huduma mbalimbali pamoja na kumsaidia kupata matokeo chanya kupitia sekta ya Kilimo ambayo serikali imekuwa ikisistiza watanzania katika nyanja hiyo ili kuendelea kujikimu katika maisha"
"Tumeona kuwa serikali ya awamu ya sita imeweza kutoa kipaumbele katika sekta ya Kilimo hivyo sisi kama wadau wa kilimo tumekuja na kampeni ya Mtumishi shambani ambapo tunatoa huduma pale mteja anaponunua vifaa kwetu , kumwezesha kupata mikopo kupitia sekta ya kifedha ili kuwasaidia wafanyakazi na Watumishi wa Umma wawze kufanya kilimo chenye tija"
Mashindano hayo ya SHIMIWI ambayo yanahusisha michezo ikiwemo ya mpira wa miguu, kuvuta kamba , mbio za baiskeli, riadha, Karata Draft yameanza October 2 yanaendelea katika viwanja mbalimbali jijini Tanga huku ukitarajiwa kuhitimishwa October 15 yakibebwa na kauli mbiu isemayo 'mazoezi mahala pa kazi huondoa magonjwa yasiyoambukiza.
MAMLAKA ZA AJIRA ZAAGIZWA KUENDELEA KULIPA WATUMISHI STAHIKI ZAO KISHERIA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 05, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 05, 2022
Rating:








Post a Comment