MDH YAKABIDHI VIFAA MUHIMU VYA KUKABILIANA NA UGONJWA WA EBOLA
Katika jitihada za kuongeza uelewa wa hatua za kujikinga na ugonjwa wa Ebola, Menejimenti na Maendeleo ya Afya (MDH kwa ufadhili wa Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Marekani (CDC) wamekabidhi vifaa muhimu vya kukabiliana na mlipuko na vipeperushi vya elimu vya kuhabarisha umma kuhusiana na ugonjwa wa Ebola ili kuunga juhudi za Kitaifa katika kuzuia ugonjwa huo kuingia nchini.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo kwa Waziri wa Afya, Mhe Ummy katika Soko la Kimataifa la Ndizi Murongo mpakani mwa Tanzania na Uganda.
“Tutaendelea kutoa elimu kwa umma, kwa watendaji wote wa Vijiji, Kata na Tarafa pamoja na kutoa mafunzo kwa waganga wa tiba asilia ili kutambua mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola.
Tutaupa kipaumbele Mkoa wa Kagera katika kukabiliana na tishio hili, kwani Mkoa huu eneo kubwa linapakana na nchi nyingi”
Vifaa hivyo vilivyopokelewa leo vitasambazwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya za mipakani mkoani Kagera
MDH YAKABIDHI VIFAA MUHIMU VYA KUKABILIANA NA UGONJWA WA EBOLA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 06, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 06, 2022
Rating:





Post a Comment