Header AD

header ads

Mhe. Mchengerwa apongeza Serengeti Girls kufuzu robo fainali Kombe la Dunia.




Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Soka ya Taifa wasichana U17 ( Serengeti Girls)kwa kufuzu  kuingia robo fainali baada ya kufungana bao 1-1  na Canada katika mechi iliyoisha hivi punde kwenye mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini India 

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa  mechi hii Mhe. Mchengerwa amesema  wachezaji wameonesha  uzalendo mkubwa kwa Taifa lao, na kusisitiza kuwa wanatakiwa kuendelea na uzalendo  huo wa kucheza kufa na kupona ili kurejesha kombe nyumbani.


"Kwa niaba ya Serikali ninapenda kupongeza Sana timu yetu ya Serengeti Girls kwani  wametambua kuwa wana wajibu mkubwa wa  kuiwakisha Tanzania  katika mashindano haya" amefafanua Mhe Mohamed Mchengerwa


Aidha, amesema ushindi huo umetokana  na mchango mkubwa na msukumo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan anaoutoa katika Sekta za Michezo hapa nchini.

" Hapa ni lazima nimshukuru Mhe. Rais  kwa maelekezo ya mahususi na kipaumbele anachotoa kwenye sekta hii" ameongeza Waziri Mchengerwa.


Kwa matokeo ya sasa Tanzania imefuzu Robo  Fainali Kombe la Dunia la Wanawake  chini ya Miaka 17 baada ya kuitoa Canada baada ya kupata sare ya Goli 1- 1 katika mechi ya Kundi D Uwanja wa DY Patil Mumbai.

Pia Kwa matokeo haya,  Tanzania Sasa inaungana na Japan katika hatua ya Robo fainali ya michuano hiyo Kwa Kundi D.

Amewaomba watanzania kuiombea timu hiyo ili iweze kuendelea kushinda.


Mhe. Mchengerwa apongeza Serengeti Girls kufuzu robo fainali Kombe la Dunia. Mhe. Mchengerwa apongeza Serengeti Girls kufuzu  robo fainali Kombe la Dunia. Reviewed by Fahadi Msuya on October 18, 2022 Rating: 5