Header AD

header ads

NIC , BODI YA USIMAMAMIZI WA STAKABADHI ZA GHALA KUTATUA CHANGAMOTO KWENYE UNUNUZI WA KOROSHO

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu na Mkurugenzi Mtendaji wa NIC,Dkt. Elirehema Doriye wakionesha mkataba waliosaini wa makubaliano kutoa huduma za Bima kwenye zao la korosho kwa msimu wa 2022/2023 ili kuwasaidia wakulima wa zao hilo nchini. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 10,2022 Jijini Dar es Salaam

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa NIC,Dkt. Elirehema Doriye wakisaini mkataba wa makubaliano kutoa huduma za bima katika zao la Korosho kwa msimu wa 2022/2023 ili kuwasaidia wakulima wa zao hilo nchini. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 10,2022 Jijini Dar es Salaam.


Na Yusuph Digossi

Katika kutatua changamoto kwenye ununuzi wa zao la korosho Nchini Tanzania Shirika la Bima la Taifa ( NIC) limesaini mkataba wa makubaliano na Bodi ya usimamamizi wa stakabadhi za Ghala .

Mkataba huo wa makubaliano umesainiwa Leo Jumatatu Oktoba 10, 2022 katika Ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam ambao utajikita katika kutoa huduma za bima kwenye zao la korosho kwa msimu wa 2022/2023.

Akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Dkt. Eliherema Doriye amesema kuwa wameingia makubaliano hayo ili kuwasaidia wakulima wa zao la korosho Nchini Tanzania.


"Bima hii itahusisha kulipa gharama za ajali ya moto zitakazokuwa zinatokea maghala ambapo awali wakulima na wafanyabiashara wa zao la korosha walikuwa wanapata changamoto kutokana na baadhi kutokuwa na bima ya mazao yao" amesema Doriye 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu, amesema makubaliano hayo yataimarisha utendaji wa mfumo wa Stakabadhi za Ghala nchini kwa kuondoa kero ya malipo kwa wanunuzi baada ya kukosa mzigo kamili ghalani.


"naombe niwakumbushe wanunuzi wote nchini kuhakikisha hawafanyi uzembe wa makusudi wakitegemea kuna bima ambayo wamekata kwani wakifanya hivyo watajiondolea uaminifu" amesema Bangu



NIC , BODI YA USIMAMAMIZI WA STAKABADHI ZA GHALA KUTATUA CHANGAMOTO KWENYE UNUNUZI WA KOROSHO NIC , BODI YA USIMAMAMIZI WA STAKABADHI ZA GHALA KUTATUA CHANGAMOTO KWENYE UNUNUZI WA KOROSHO Reviewed by Fahadi Msuya on October 10, 2022 Rating: 5