Header AD

header ads

SALIM: WAANDISHI BADO HAWANA UELEWA MPANA WA SHERIA ZINAZOWAHUSU

Mumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Salim Said akizungumza wakati akifungua siku ya pili ya warsha ya kuwajengea uwezo wahariri juu ya mipango ya uchechemuzi wa marekebisho ya sheria za habari.



Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Salim Said Salim amesema bado waandishi wa habari hapa nchini hatujawa na uelewa mpana wa sheria zinazotuhusu na kufanya  jitihada kuzijua sheria hizo.


Amesema ni muhimu kwa wanahabari hapa nchini kusoma sheria mbalimbali zimazohusu tasnia ya habari na nyingine ili wanapopiga kelele zirekebishwe kuwe na ushawishi.

Salim Said Salim aliyasema hayo  Ijumaa Oktoba 21, 2022  wakati akifungua warsha ya kuwajengea uwezo wahariri juu ya mipango ya uchechemuzi wa mabdiliko ya sheria za habari.

 "mwandishi wa habari akijua haki zake, sheria zinazoongoza tasnia ya habari ataweza kukutana na makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo wabunge na kuwashawishi juu ya sheria zinaminya uhuru wa habari na haki za binadamu" amesema 


kwa upande wake mwezeshaji Tumaini Mbibo, amesema ni muhimu kwa waandishi wa habari kujua kiini cha matatizo yanayolikabili Taifa na njia za kutumia ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo husika.

Amesema haki za binadamu zinakwenda sambamba na demokrasia hivyo uwepo wa sheria zinazominya tasnia ya habari zinakwamisha maendeleo hivyo vema ikafanyika mipango ya kufanya ushawishi wa mabadiliko.



SALIM: WAANDISHI BADO HAWANA UELEWA MPANA WA SHERIA ZINAZOWAHUSU SALIM: WAANDISHI BADO HAWANA UELEWA MPANA WA SHERIA ZINAZOWAHUSU Reviewed by Fahadi Msuya on October 22, 2022 Rating: 5