SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 IMEFANYIKA KWA UFANISI: ANNA MAKINDA
Na Hadija Bagasha Tanga,
Kamisaa wa sensa ya watu na makazi 2022 Anna Makinda amesema sensa ya watu na makazi imefanyika kwa ufanisi nkubwa na utakuwa na tija kubwa kwa Taifa huku akieleza ugonjwa walionao watanzania sio kwamba hakuna kazi bali ni wa kifikra wa kwamba elimu ni kuajiriwa bila kudhani kwamba ni ufunguo wa maisha.
Kamisaa Makinda ameyasema hayo wakati alipokuwa akipokea taarifa ya utekelezaji wa zoezi la Sensa ya watu na makazi ambalo lilifanyika Augost 23 mwaka huu ambapo ameeleza kuwa zoezi hilo limefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90 nchini kote hii ikiwa ni kutokana na elimu iliyotolewa kwa wananchi ambao wameonyesha ushirikiano kwa makarani wa sensa kote nchini.
Kamisaa Makinda amesema ndio maana Rais ameweka nguvu kubwa kwa wamachinga kwasababu nfio sekta inayochukua watu wengi hapa nchini na amewawekea mipango mizuri ambayo ataiwrka wazi hapo baadaye mara baada ya kutangaza matokeo ya idadi ya watanzani.
Amesema kwamba kada ya umachinga imekuwa ndio kimbilio la vijana wengi kwa kuwe wengi wao wamejiajiri wenyewe na hivyo kuchochea pato la mtu mmoja mmoaja na Taifa kwa ujumla bila kusubiri kuajiriwa.
"Tunachokisema ugonjwa tulionao sisi sio kazi hazipo tunaugonjwa wa mindset lakini pia tuna ugonjwa wa tafsiri elimu sio kuajiriwa elimu ni ufunguo wa maisha kwahiyo unakuta mheshimiwa Rais hapa kwenye sensa hii ameweka nguvu sana kwa machinga nguvu sana na anasubiria baada ya sensa hii afanye mambo yake aliyoyafanya kwa machinga, "alisisitiza Kamisaa Makinda.
Aidha Kamisaa Makinda amesema serikali kupitia tume za Taifa za Takwimu Tanzania bara na visiwani Zanzibar imelenga kutumia takwimu za watu zilizopatikana kwenye Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kujiajiri ili kuondokana na tatizo la ajira hapa nchini.
"Ofisi zetu ya takwimu Tanzania bara na Zanzibar wanaandaa mpango wa kutoa elimu kuhusu matokeo ya sensa ilivyofanyika,takwimu zilizopatikana itabidi zifanye kazi mara baada ya Rais kuitangaza kutakuwa na program za kufundisha wananchi maana ya tawimu zile kusudi zitumike katika kazi zote kuanzia ngazi kitongoji na hadi Taifa , ikiwemo taarifa za ni wapa hakuna huduma za kijamii tunatamani sana hii sensa itumike katika mabadiliko" alisema Makinda.
"Takwimu zetu safari hii tunataka zifanye kazi , mheshimiwa Rais ameweka nguvu kubwa sana kwa wamachinga , machinga itakuwa ndio sekta ambayo itachukuwa watu wengi sana hivyo katika sensa hii kuna kila kitu kuna mahali inaonyesha kabisa vijana wetu waliosoma na wapo nyumbani kwa muda mrefu , ugonjwa tulio nao sisi sio kazi hazipo bali tuna ugonjwa wa tafsiri elimu sio kuajiriwa bali ni ufunguo wa maisha" alieleza.
Awali akieleza namna sensa ilivyofanyika kwa mkoa wa Tanga mratibu wa mkoa huo Tony Mwanjota alisema kuwa wameweza kufanikiwa kuhesabu kaya kwa asilimia 95 na kuyafikia majengo yote, kuiwezesha kutoa elimu na hamasa kwa wananchi ambayo imepelekea ushirikiano mkubwa uliochangiwa na viongozi wa serikali dini na siasa .
"Tumeweza kufanikiwa kuhesabu kaya kwa asilimia 95 na kuyafikia majengo yote pia kuwezesha wananchi kuwa na elimu na hamasa ya kutosha kuhusu zoezi , mafanikio haya yametokana na viongozi wa dini serikali na sisasa , na kutokana na hamasa waliyokuwa nayo hatukutumia nguvu ya dola kumlazimisha mtu ahesabiwe bali wananchi wenyewe " alisema Mwanjota.
Aidha ameeleza baadhi ya changamoto walizokutana nazo makarani wa sensa zikiwemo ugumu wa kupata taarifa ikiwemo taarifa za uzazi na elimu kwa, kuchelewa kufika kwa vifaa kuletwa kwa mafungu pamoja na waratibu wa ngazi za wilaya kukosa mafunzo kikamilifu kutokana na zoezi la usaili wa makarani hivyo kushindwa kufikia lengo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba ameeleza kuwa wanaendelea kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutenga maeneo maalumu kwaajili ya kilimo ili kutumia sekta ya Kilimo katika kuwakwamua wananchi na umasikini na kuwa na chakula toshelevu wakati wote ili kuweza kuchangia pato la taifa.
"Tunaendelea kuyafanyia kazi maelekezo ya Rais aliyosema tutenge kila mkoa hekali zisizopungua laki moja na hamsini kwaajili ya kilimo hususani mazao yale ambayo tunakwenda zinazotukabili katika taifa letu mfano mazoa yenye asili ya mafuta maeneo hayo tayari tumeyatenga na tumeshazielekeza ofisi zetu za wilaya kutenga maeneo hayo " alisema Mgumba.
"Kuna uvamizi wa maeneo lakini tumeshatoa maelekezo tuyabaini hayo maeneo na watu husika tuwape elimu na kuwaondoa na kwababu hili linakuja sambamba na migogoro ya ardhi katika mkoa wetu ikiwemo wananchi kuvamia maeneo ya viwanda na uwekezaji"
SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 IMEFANYIKA KWA UFANISI: ANNA MAKINDA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 07, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 07, 2022
Rating:







Post a Comment