SIMBACHAWENE ASISITIZA UCHAGUZI HURU, HAKI NA UNAOZINGATIA USAWA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene akifungua warsha ya siku nne ya kujengea uwezo Tume za Uchaguzi na wadau wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) tarehe 25 Oktoba, 2022, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi (Elimu ya Mpiga Kura) Bi. Monica Mnanka akiwapa maelezo baadhi ya washiriki wa warsha ya siku nne ya kujengea uwezo Tume za Uchaguzi na wadau wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) kuhusu machapisho mbalimbali ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Na Mwandishi wetu- Da r es Salaam
Na Mwandishi wetu- Da r es Salaam
Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri Mkuu Anayeshughulikia Masuala ya sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene amesema bado kuna haja kubwa ya nchi wanachama wa maziwa makuu kuhakikisha kwamba chaguzi zinakua huru, za haki na zenye kuaminika ambayo itasaidia kwenye kukuza demokrasia itakayochochea amani, usalama na ustawi wa wananchi.
Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam, wakati wa warsha iliyokutanisha nchi wanachama 12 ikiwemo Angola, DR Congo, Kenya, Rwanda, Burundi, South Sudan, Zambia na Sudan na taasisi zinazosimamia chaguzi katika nchi kwa maana ya tume za uchaguzi ili kupeana uelewa na kungalia changamoto zinazoikumba Masuala ya kuendesha chaguzi.
"Wamekutana wamepeana uelewa, wameangalia changamoto zinazoikumba masuala ya kuendesha chaguzi kuanzia kuandaa, kusimamia na kutangaza matokeo ya uchaguzi ambapo wanabadilishana mawazo na kupeana uzoefu lakini pia kujaribu kusahihisha baadhi ya changamoto"
Simbachawene alisema katika maeneo ya nchi nyingine wananchama wa nchi za maziwa makuu hali zinatofautiana kuna wengine kila inapofikia uchaguzi ni lazima nchi ivunjike ambapo wakimaliza uchaguzi wanaanza kuitengeneza nchi upya na mwisho wa siku anayepata hasara ni mwananchi ambaye shida yake alitegemea kupata huduma bora ya kijamii, barabara, huduma za afya, elimu n.k
Aidha Simbachawene alisema Uchaguzi ni sehemu ya shughuli ya msingi lakini mwisho wa siku lazima wahakikishe kwamba nchi inabaki kuwa na amani.
"Hekima moja na ya upekee katika uchaguzi ni ile ya uzalendo wa amani na utulivu wa nchi kwasababu mwisho wa siku tutahitaji kwenda mashambani, kazini n.k hivyo amani ikitoweka hatutoweza kuwa huru"
Pia Simbachawene alisema Kwa Tanzania wameweza kufanya chaguzi mbalimbali na walifanikiwa kumaliza vizuri ambapo vyombo vya ulinzi na usalama vimeonekana kuwa muhimu katika kipindi hicho hasa jeshi la polisi kwa kuhakikisha chaguzi inafanyika na kumalizika kwa amani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Charles Mahera, alisema Masuala yatakayoshughulikiwa katika warsha hiyo ni kuboresha uadilifu wa uchaguzi unaoshirikisha makundi yote katika jamii kama vile wanawake, wazee, vijana na watu wenye ulemavu.
Pia Dkt. Mahera alisema "zitashughulikiwa changamoto, fursa na matumizi ya TEHAMA katika chaguzi, changamoto na fursa zilizopo katika kuboresha ushiriki wa vijana katika uchaguzi kama wagombea na wapiga kura lakini pia changamoto na fursa zilizopo katika kuboresha ushiriki wa watu wenye ulemavu katika chaguzi, nafasi za asasi za kiraia katika kuboresha ushirikia wa makundi maalum na uadilifu wa vyombo vya habari katika mchakato wa uchaguzi ili kuhakikisha kunakua na amani na utulivu"
Kadhalika Dkt. Mahera alisema Watajadili changamoto za uchaguzi za nchi wanachama na athari za majanga mbalimbali kama vile ugonjwa wa COVID-19 na ukame n.k
Mbali na hayo Dkt. Mahera alisema Kutakua na njia za kutatua malalamiko yanayotokana na uchaguzi kwa amani na maridhiano ili kuendelea kudumisha amani na demokrasia na maendeleo kwa wananchi.
SIMBACHAWENE ASISITIZA UCHAGUZI HURU, HAKI NA UNAOZINGATIA USAWA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 26, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 26, 2022
Rating:







Post a Comment