TANROADS: BAADHI YA SEHEMU ZA BARABARA YA KIDAWE- NYAKANAZI ZIMEJENGWA KWA FEDHA ZA NDANI
Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila akitoa taarifa ya miradi kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla za Ufunguzi wa Barabara ya KIDAHWE-KASULU( Km. 63)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine wakati akivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa Majengo mapya ya chuo cha Ualimu Kabanga, kilichopo Kasulu Mkoani Kigoma tarehe 17 Oktoba, 2022
Na Yusuph Digossi
Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila amesema kuwa baadhi ya sehemu za Barabara ya kutoka Kidawe hadi Nyakanazi ambazo ni Kidawe, Kasulu, na sehemu ya kibondo zimejengwa kwa fedha za ndani.
Mhandisi Rogatus Mativila ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya miradi kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla za Ufunguzi wa Barabara ya KIDAHWE-KASULU( Km. 63), na uwekaji jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya KABINGO-KIBONDO KASULU- MANYOVU ( Km. 260.6) .
Hafla hii imefanyika mapema leo Oktoba 17, 2022 Wilayani Kasulu, Mkoani Kigoma.
Kuhusu Barabara ya Kidawe Kasulu ambayo imekamilika Mhandisi Mativila amesema imejengwa na kampuni ya China Railway 15 Beaureau group ( CR15) kwa gharama ya shilingi Bilioni 64.7 na kusimamiwa na Mhandisi mshauri kwa gharama za shilingi Bilioni 5.7.
Kwa upande wa barabara ya Kabingo- Kasulu Mhandisi Mativila amesema Barabara hiyo inayounganisha Mikoa ya jirani kama vile Mikoa ya Kagera, Shinyanga, Geita na Mwanza na nchi jirani ya Burundi kupitia mpaka wa manyovu imekua ikipitika kwa shida kipindi cha mvua hivyo imefikia mahala inabidi ijengwe.
Amesema ujenzi wa barabara hiyo ni mkakati wa Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara kuu zinazounganisha Mikoa na kuunganisha Tanzania na nchi jilani na kujenga kwa kiwango cha lami barabara za mikoani.
TANROADS: BAADHI YA SEHEMU ZA BARABARA YA KIDAWE- NYAKANAZI ZIMEJENGWA KWA FEDHA ZA NDANI
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 17, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 17, 2022
Rating:


Post a Comment