Header AD

header ads

VIJANA TANGA WAHIMIZWA KUDHURIA MAFUNZO YA KUPATIWA MIKOPO



Na Hadija Bagasha Tanga, 

Halmashauri ya jiji la Tanga imewahimiza vijana jijini Tanga kwenda kupata mafunzo na kuelekezwa namna ya kuomba mikopo itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi na badala yake waache kutumia nguvu zao na maarifa yao kwenda kwenye makundi ya watoto wa ibilisi na panya rodi. 

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugemzi wa Halmashauri ya jiji la Tanga Dkt. Spora Liana wakati wa kikao cha baraza la, madiwani wa Halmashauri ya jiji hilo. 


Mkurugenzi Liana amesema wanaendelea kuhamasisha vijana,  wakinamama na watu wenye ulemavu ili waweze kwenda kuchukua mikopo kwani wataalamu wamepangwa ili waweze kuwasaidia kupata mikopo ya asilimia 10 isiyokuwa na riba. 

"Mheshimiwa Rais Samia amerahisisha sana ameweka mazingira wezeshi mazuri sana katika nchi hii kwahiyo waje kuchangamkia fursa hii na leo hii tumetoa mikopo ya zaidi ya milioni 300 kwajili kukamilisha mikopo itakayotolewa kwa mwaka uliopita, "alisistiza Dkt Liana. 


Aidha Dkt Liana amesema kuwa mikopo wanayotarajia kuitoa ni ya zaidi ya bilioni 1 hivyo amewahimiza wakazi wa jiji la Tanga wenye familia zao kuhimizana kwajili ya kupata mafunzo na kuelekezwa namna ya kuomba mikopo hiyo. 

"Vijana waleteni sisi tutawaelekeza tuna programs nyingi sana tumeziandaa za vijana tunajua vijana wana nguvu wana maarifa,  vijana wasitumie nguvu zao na maarifa yao kwenda kwenya makundi ya watoto wa ibilis, kwenya makundi ya panya rodi waje hapa watumie kwajili ya uzalishaji na kuweza kuuza matunda,  mboga,  mazao na bidhaa mbalimbali tuna mchakato wa kuwaunganisha na masoko na pia tunaandaa eneo la ekari 200 ili waweze kulima kilimo cha umwagiliaji, "alibainisha Dkt Liana. 

Aidha Dkt Liana amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia shilingi milioni 380 kwajili ya ujuenzi wa madarasa 29 katika Halmashauri ya jiji la Tanga jambo ambalo halijawahi kutokea. 

"Mwaka jana katoa fedha na mwaka huu pia katoa hii haijawahi kutokea katika Nchi hii na sisi pamoja na waheshimiwa wataalamu madiwani na wananchi wa jijila Tanga tunamuunga mkono na tuko tayari kutekeleza maagizo yake ya kuweza kujenga madarasa na kukamilisha kwa muda unaotakiwa, "alisema Dkt Liana

Aliongeza kuwa Mheshimiwa Rais ameagiza hadi kufikia tarehe 31 desemba hayo madarasa yawe yamekamilika lakini mkuu wa Mkoa ameagiza mpaka tarehe 15 Novemba hayo madarasa yawe yamekamilika hivyo tunahakikisha zile pesa zinaingizwa katika vifungu ili tuwezs kuanza ujenzi mara moja. 

Awali akizungumza katika kikao hicho Mstahiki Meya wa jiji hilo Abdulrahman Shiloo amekazia kwenye suala la miradi na kueleza kuwa hivi sasa wana miradi ya madarasa 29 ambayo wamepata fedha kiasi cha shilingi milioni 580 kutoka Rais kwajili ya kuepuka uhaba wa madarasa kwenye mwaka wa masomo 2023.


"Nikuombe Mkurugenzi na wakuu wake wa idara kuhakikisha kwamba madarasa hayo yanakamilika kama tulivyoelekezwa na ofisi yetu ya Mkuu wa Mkoa kwamba tarehe 15 sasa haya yatafanikiwa ikiwa sisi waheshimiwa madiwani ambao kwenye kata zetu shule hizi zipo tutatoa ushirikiano wa kutosha kwahiyo niwaombe waheshimiwa madiwani wazisimamie shule hizi na watoe ushirikiano wa kutosha kama kuna changamoto tuzitatue mapema, "alisema Meya Shiloo. 

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ngamiani Kaskazini Fahad Abdallah amesema kiasi hicho cha fedha alichokitoa mheshimiwa Rais ni jambo jema hivyo ameshauri ujenzi wa madarasa hayo usicheleweshwe ili kuendelea kumtia moyo Rais Samia. 

"Sisi kama Halmashauri na kamati tutapita kwenye hayo madarasa kuhakikisha tarehe zilizowekwa zinafwatwa, "alisema Diwani Fahad. 

Hata hivyo  Diwani Fahad ameiomba Halmashauri ya jiji hilo kuhakikisha inatekeleza yale aliyoyaahidi kwenye kampeni yake ikiwemo kuboresha miundombinu ya barabara na taa katika kata hiyo ili kuendelea kutekeleza ilani ya chama hicho. 




VIJANA TANGA WAHIMIZWA KUDHURIA MAFUNZO YA KUPATIWA MIKOPO VIJANA TANGA WAHIMIZWA KUDHURIA MAFUNZO YA KUPATIWA MIKOPO Reviewed by Fahadi Msuya on October 28, 2022 Rating: 5