Header AD

header ads

WAZIRI AWESO AIPONGEZA RUWASA KWA KUWA NAMBA MOJA KWA UTEKELEZAJI WA UBORA WA MIRADI WAKATI WA MBIO ZA MWENGE


Waziri wa Maji Jumaa Aweso akifungua mafunzo ya maadili ya utumishi wa Umma, uongozi na taaluma pamoja na elimu ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa Menejimenti ya RUWASA yanayoendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi  Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement Kivegalo akizungumza wakati wa mafunzo ya maadili ya utumishi wa Umma, uongozi na taaluma pamoja na elimu ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa Menejimenti ya RUWASA yanayoendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam.


Na Yusuph Digossi- Dar es Salaam 

Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameipongeza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ( RUWASA) kwa kasi ya kutekeleza miradi ya kupeleka maji Vijijini na kutajwa kuwa namba moja kwa utekelezaji na ubora wa miradi katika ukaguzi uliofanywa wakati wa mbio za mwenge.

Waziri Aweso ametoa pongezi wakati akifungua mafunzo ya maadili ya utumishi wa Umma, uongozi na taaluma pamoja na elimu ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa Menejimenti ya RUWASA .

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo yanayoendelea katika ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam Waziri Aweso emesema siri ya mafanikio hayo katika sekta hiyo iliyopo chini ya Wizara ya maji ni kufanya kazi kwa bidii, uaminifu, uadilifu, na kwa kuzingatia weledi.

" Nawapongeza Sana RUWASA kasi na ubora wa kutekeleza miradi ya Maji Vijijini na kupelekea sekta ya Maji kuwa namba moja kwa utekelezaji na ubora wa miradi katika ukaguzi uliofanywa wakati wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka huu" amesema Waziri Aweso


Kwa upande wake Mkurugenzi  Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement Kivegalo kuwa mafunzo hayo  amesema  kuongeza weledi, uaminifu na uadilifu zaidi kwa watumishi hao ikiwa ni njia mojawapo ya kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi.

Alisema sekta hiyo hususan eneo la Maji Vijijini limepiga hatua nzuri kiasi cha kutangazwa na timu ya wakimbiza Mwenge Kitaifa kuwa namba moja nchini na kusema kuwa "hii ni ni changamoto mpya kwangu kama mtendaji Mkuu na kwa watumishi wote wa RUWASA kuzidisha bidii ya kazi kwa weledi mkubwa" 

WAZIRI AWESO AIPONGEZA RUWASA KWA KUWA NAMBA MOJA KWA UTEKELEZAJI WA UBORA WA MIRADI WAKATI WA MBIO ZA MWENGE WAZIRI AWESO AIPONGEZA RUWASA KWA KUWA NAMBA MOJA KWA UTEKELEZAJI WA UBORA WA MIRADI WAKATI WA MBIO ZA MWENGE Reviewed by Fahadi Msuya on October 28, 2022 Rating: 5