WAZIRI GWAJIMA ASHIRIKI MJADALA WA JUKWAA LA WASICHAMA " GIRLS AJENDA "
Waziri Dkt.. Gwajima ameshiriki mjadala katika Jukwaa la Msichana "Girl Ajenda Forum 2022" lililoandaliwa na Wadau mbalimbali kwa lengo la kusikiliza Masuala yanayowahusu wasichana kuelekea maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mtoto wa kike inayofanyika kila Oktoba 11.
Katika Jukwaa hilo mambo yaliyojitokeza ni pamoja na suala la mkanganyiko wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 na sheria ya Mtoto (1999) hususani kuhusu umri wa kuolewa.
Suala lingine ni gharama ya taulo za kike ambapo wasichana wameiomba Serikali kupunguza tozo kwa taulo hizo au kuondolewa kabisa kwa sababu wengi wao hasa maeneo ya vijijini wanashindwa kumudu gharama hizo hivyo kushindwa kuhudhuria masomo wakiwa ktika siku za hedhi.
Akizungumza katika Jukwaa hilo Waziri. Dkt. Gwajima amesema suala la sheria ya ndoa limeanza kufanyiwa kazi na Kamati maalum kupitia Wizara ya Katiba na Sheria, hatua iliyopo ni kukusanya maoni ya wananchi ili kuwa maamuzi ya pamoja kama nchi.
Aidha kuhusu tozo kwa taulo za kike amesema amelipokea, ataliwasilisha kwenye Wizara ya Fedha na Mipango ambayo ina dhamana ya tozo ili itoe maelekezo, pia amebainisha ipo haja ya kuwa na viwanda vya taulo za kike ndani ya nchi na ni fursa kwa wawekezaji wa ndani na wanawake hasa kupitia mabaraza ya uwezeshaji Wanawake kiuchumi.
WAZIRI GWAJIMA ASHIRIKI MJADALA WA JUKWAA LA WASICHAMA " GIRLS AJENDA "
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 11, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 11, 2022
Rating:




Post a Comment