Waziri Mchengerwa awapongeza Serengeti Girls Kwa kuibamiza Ufaransa.
Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Soka ya Wanawake Serengeti Girls Kwa kuibamiza timu ya Ufaransa mabao 2-1 katika mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini India.
Mhe. Mchengerwa amesema wachezaji wameonesha uzalendo mkubwa kwa nchi yao na amewataka kuendelea kucheza kufa na kupona katika mechi zilizosalia ili kurejesha kombe nyumbani.
Aidha, amesisitiza kuwa Serikali ipo pamoja na timu hiyo katika kila hatua ili kuhakikisha inarudi na kombe nchini.
Amewaomba watanzania kwa umoja wao waiombee timu hiyo ili hatimaye ishinde mechi zilizobaki. Na kutwaa kombe.
Magoli ya Tanzania yamefungwa na Diana Mnaly na Christer Bahela.
Kwa matokeo hayo Tanzania inakamata namba 2 nyuma ya Japan na nafasi ya tatu Canada na nne ni Ufaransa, huku ikiwa na mechi Moja mkononi dhidi ya Canada itakayochezwa Oktoba 18, 2022 jijini Mumbai, India.
Mhe. Mchengerwa ametoa wito kwa
Uchungizi umebaini wananchi wengi nchini wamekuwa wakifuatilia mtanange huo, huku wakiwaombea waendelee kushinda.
Waziri Mchengerwa awapongeza Serengeti Girls Kwa kuibamiza Ufaransa.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 15, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 15, 2022
Rating:



Post a Comment