WAZIRI UMMY AWATAKA WATANZANIA KUVUNJA UKIMYA NA KUZUNGUMZA KUHUSU AFYA YA AKILI
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa wito kwa jamii kuvunja ukimya na kuzungumza kuhusu afya ya akili kwakua ipo changamoto ya Afya ya akili kwenye jamii kutokana na maendeleo ya Teknolojia huku akibainisha kuwa tatizo hilo linaweza kumpata mtu yoyote na halichagui umri jinsia au kipato cha mtu.
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo wakati akifungua Kongamano la kwanza la Kitaifa la Afya ya akili lenye kauli mbiu " afya ya akili kipaumbele kwa wote" lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam Leo Jumatatu Oktoba 10 2022.
Akizungumza wakati akifungua Kongamano hilo amesema Kwakuwa Afya ya akili ni kipaumbele kwa wote kongamano hili linalenga kuhamasisha Serikali, Jamii na wadau wa maendeleo kujadili nini kimefanyika na nini kinapaswa kufanyika ili kupunguza tatizo hili nchini.
"Tuvunje ukimya tuzungumze kuhusu Afya ya akili kwa kuwa ipo changamoto ya Afya ya akili kwenye jamii zetu kutokana na maendeleo ya tekinolojia." amesema Waziri Ummy
Waziri Ummy amebainisha kuwa magonjwa ya akili yameongezeka, ambapo takwimu za kidunia zinaonesha kuwa katika ya watu nane mtu mmoja anatatizo la akil
Vilevile Waziri Ummy alitaka uwepo wa huduma za afya ya akili na wataalamu kupatikana kuanzia ngazi ya zahanati hadi Hospitali ya Taifa na pia uwepo na vituo ambavyo watu watapata huduma hizo.
Katika hatua nyingine Ummy Mwalimu ametoa Tuzo ya Ubalozi wa masuala ya Afya ya Akili kwa Mhe. Jesca Msambatavangu (Mbunge wa Iringa Mjini) kwa kuthamini mchango wake wa kuibua na kujadili masuala ya Afya ya Akili pamoja na kuchangia mijadala mbalimbali yenye lengo la kuibua mada mbalimbali za kujadili masuala ya Afya ya Akili hadi kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
WAZIRI UMMY AWATAKA WATANZANIA KUVUNJA UKIMYA NA KUZUNGUMZA KUHUSU AFYA YA AKILI
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 10, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 10, 2022
Rating:




Post a Comment