Header AD

header ads

BENKI YA KCB YAZINDUA HATIFUNGANI YA 'SUKUK' WATANZANIA KUWEKEZA KWA MTAJI WA LAKI 5 TU



Benki ya –KCB  imekusudia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 10 kuanzia Novemba 9 hadi Disemba 5 mwaka huu kupitia hati fungani bila riba iliyopewa jina la fursa Sukuk lengo ni kuisaidia serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza  Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa awali wa mauzo ya hatifungani, Mkurugenzi wa usimamizi wa sekta ya fedha kutoka benki kuu nchini –BOT, Sadat Musa amesema juhudi zilizofanywa na –KCB imeunga mkono dhamira ya serikali katika kupunguza umaskini kwa watanzania.


"Ni dhahiri kuwa juhudi hizi zinaendana na malengo ya serikali ya kukuza uchumi pamoja na kupunguza umasikini kwa wananchi kupitia upatikanaji wa kutosha na kwa gharama ambayo wananchi wanaweza kuimudu" Alisema Sadati na kuongeza kuwa 

"Serikali kupitia benki kuu ya Tanzania imechukua hatua mbalimbali ili kuiwezesha mabenki kuwa na ukwasi wa kutosha kwaajili ya kutoa mikopo kwa wananchi wote hatua hizo ni pamoja na kupunguza viwango vya uwekaji sehemu ya amana benki kuu, kuongeza uiano wa matumizi ya hati fungani"


Aidha alisema anategemea benki zote zitumie fursa hizo vizuri ili kuendelea kupunguza gharama za riba za mikopo itolewayo kwa wateja wake na wananchi kwa ujumla.


"Hii inawezekana kwa kuongeza ubunifu kama ambavyo tumeshuhudia kwa KCB katika utoaji wa huduma za kibenki ikiwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia kwaajili ya kuwafikia wananchi wengi zaidi hasa waliopo maeneo ya vijijini"

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki y KCB, Cosmas Kimario alisema hati fungani hiyo imelenga kukusanya fedha kiasi cha shilingi bilioni 10 ambazo zitatumika kuendeleza idara ya KCB inayotoa huduma za kiislamu ikiwemo mikopo , huduma za miamala za kibenki na uwekezaji.


"Huu ni uwekezaji wa uhakika ambao unakupa gawio la faida la asilimia 8.75 kwa mwaka ambao gawio litatolewa mara nne kwa mwaka (mara moja kila robo mwaka) , mtu yoyote anaweza kununua hati fungani ya Fursa Sukuk kwa kiwango cha kuanzia shilingi laki tano na kuendelea "

Aidha Kimario aliwakaribisha watanzania kuchangamkia fursa hiyo ya uwekezaji ambayo inampa mwekezaji thamani halisi ya pesa na kwa muda mfupi wa miaka mitatu"

Naye Mkuu wa Idara ya Huduma za kibenki za kiislamu Sahl Banking, Amour Muro alisema zinazokusanywa kwa wawekezaji zitatumika katika biashara au huduma zinafouta shariah na faida inayopatikana hupewa kama gawio kwa wawekezaji.



"Faida itakayopatikana kupitia hizi huduma za KCB Sahl Banking itatolewa kama gawio kwa wawekezaji kupitia mkataba wa mudharaba. Mkataba wa Mudharaba ni aina ya ushirikiano ambapo mteja anachangia mtaji na benki inasimamia hazina hiyo ili kuzalisha faida. Faida hugawanywa kati ya mteja na benki kwa uwiano uliokubaliwa awali".alisema

Muro aliongeza kuwa watanzania watakaohitaji kuwekeza watajaza fomu za maombi zitakazopatikana katika matawi yote ya Benki ya KCB Tanzania na Benki ya CRDB Plc na ofisi za madalali na wafanyabishara wa soko la Hisa la Dar es Salaam waliopewa leseni na mamlaka husika ya mtaji na dhamana (CMSA) .

"Fursa Sukuk ofa iko wazi kuanzia tarehe 9 Novemba 2022 na itafungwa tarehe 5 Desemba 2022, baada ya muda wa awali wa ofa , Fursa Sukuk itaorodheshwa kwenye soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) " alisema


BENKI YA KCB YAZINDUA HATIFUNGANI YA 'SUKUK' WATANZANIA KUWEKEZA KWA MTAJI WA LAKI 5 TU BENKI YA KCB YAZINDUA HATIFUNGANI YA 'SUKUK' WATANZANIA KUWEKEZA KWA MTAJI WA LAKI 5 TU Reviewed by Fahadi Msuya on November 10, 2022 Rating: 5