BUSELA YAUNGA JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KUOKOA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI .
Katika juhudi za kuiunga mkono Serikali kwa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi nchini, Kampuni ya Hatua Group Afrika inayosimamia program ya Busela wameanza kuwafikia mama wajawazito kwa kuwapatia Elimu ya Afya ya Uzazi .
Akizungumza wakati wa utowaji wa elimu hiyo Novemba 07,2022 jijini Dar es Salaam iliyokwenda sambamba na ugawaji wa vifaa vya kujifungulia (Delivery Kit ) kwa mama wajawazito walio katika hatua za mwisho Mkkurugenzi mtendaji wa Hatua Group Afrika inayosimamia program ya Busela Bw. Derick Mgaya amesema mama wengi wajawazito wamekuwa hawana elimu ya kutosha kuhusu afya ya uzazi, ikiwemo utunzaji mimba, malezi, mazoezi na hata ulaji wa chakula kitendo kinachopelekea vifo vingi wakati wa kujifungua.
Aidha Bw. Derick Mgaya amesema Program ya Busela ina lengo la kuwafikia mama wajawazito zaidi ya elfu tano katika kipindi cha miezi mitatu lengo likiwa ni kutoa elimu ya Afya ya uzazi,mazoezi,jinsi ya kula vyakula pamoja na Saikolojia, ambapo kwa siku ya jana Busela wamefanikiwa kutoa elimu na kugawa vifaa vya kujifungulia kwa mama wajawazito arobaini waishio maeneo ya Vingunguti manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wao baadhi ya kinamama wajawazito walionufaika na elimu na kupatiwa vifaa vya kujifungulia kutoka Busela akiwemo Munira Zefania na Vumilia Said wote wakazi wa Vingunguti Miembeni kwa pamoja wameishukuru kampuni hiyo kwa kuweza kuwafikia nyumbani na kuwapatia elimu juu ya Afya ya uzazi pamoja na aina ya mazoezi ya kufanya huku wakitumia nafasi hiyo kuiomba serikali kupitia wizara ya Afya na wadau wengine kuunga mkono mpango huo ili uweze kuwafikia mama wajawazito wengi zaidi nchini kwani ni dhahiri kuwa mama wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu Afya ya Uzazi.
Ripoti ya mwaka 2020 iliyotolewa na WHH inaonyesha kuwa vifo vingi vya mama na mtoto katika nchi zinazoendelea vinazuilika endapo ongezeko za huduma za dharura zitatolewa ikiwemo na elimu ya kutosha.
BUSELA YAUNGA JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KUOKOA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI .
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 07, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 07, 2022
Rating:

Post a Comment