Darasa la lugha ya Kiswahili lazinduliwa Malawi
Waziri wa Elimu wa nchini Malawi,Mhe.Agnes Nyalonje leo tarehe 09/11/2022 amezindua darasa la kwanza la lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Hebron.
Akizungumza katika uzinduzi huo,Mhe. Nyalonje amesema kuwa uanzishwaji wa darasa hilo ni kati ya ushirikiano muhimu kwa nchi mbili za Tanzania na Malawi ambao utasaidia katika masuala mbalimbali.
"Ushirikiano huu ni muhimu na wenye thamani ,tutauenzi na kuhakikisha Kiswahili kinakua kwa kasi nchini kwetu"amesema Mhe. Nyalonje.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole ameeleza kuwa uanzishwaji wa darasa hilo ni muendelezo wa mahusiano mazuri ya nchi hizo na kwamba atasimamia utekelezaji katika kuhakikisha Kiswahili kinafanikiwa kukua .
Amesema kuwa huu ni mwanzo na Serikali
imani na mahusiano hayo ya vyuo yatazidi na kuimarisha mahusiano mazuri yalipo katika nchi zote.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ,Prof.Carolyne Nombo ameshukuru kwa Serikali ya Malawi kwa kukubali kuanzia ushirikiano huo na kuwa lugha ya Kiswahili itakuwa zaidi kutokana na uanzishwaji wa darasa.
Ameongeza kuwa anaamini watu wengi wa nchini Malawi wataweza kujua kwa haraka lugha ya kiswahili ambayo itawasaidia katika nyanja mbalimbali.
Darasa hilo la kwanza ,limezinduliwa leo nchini Malawi katika Chuo Kikuu cha Hebron ambapo walimu wa darasa hilo wanaofundisha kwa muda wa wiki moja wametoka katika Baraza la Kiswahili la Taifa(BAKITA).
Darasa la lugha ya Kiswahili lazinduliwa Malawi
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 09, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 09, 2022
Rating:




Post a Comment