KCB YAZINDUA HATI FUNGANI YA 'FURSA SUKUK'
Benki ya KCB Tanzania imeweka historiakwa kuzindua hati fungani inayojulikana kama 'Fursa Sukuk' inayotoa fursa ya uwekezaji kwa watanzania wote kwa mtaji wa kuanzia shilingi laki tano na kuendelea.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Cosmas Kimario wakati wa hafla ya uzinduzi, huku akisema kuwa hati fungani hiyo imelenga kukusanya fedha kiasi cha Shilingi 10 bilioni ambazo zitatumika kuendeleza idara ya KCB Sahl inayotoa huduma za Kiislamu ikiwemo mikopo, huduma za miamala za Benki, na uwekezaji.
"Huu ni uwekezaji wa uhakika ambao unakupa gawio la faida la asilimia 8.75 kwa mwaka ambapo gawio litatolewa mara nne kwa mwaka (mara moja kila robo mwaka). Mtu yoyote anaweza kununua hati fungani ya Fursa Sukuk kwa kiwango cha kuanzia Shilingi laki tano (500,000) na kuendelea," Amesema Kimario.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki za Kiislamu Sahl Banking, Amour Muro amesema fedha zinazokusanywa kwa wawekezaji zitatumika katika biashara zinazofuata sharia na faida inayopatikana zitatolewa kama gawio kwa wawekezaji.
"Hii ni hati fungani inayofuata sheria ya kiislamu, haitozi riba kutokana na faida katika biashara tunazozifanya, basi tutakuwa tunawapa wawekezaji ambao watakuwa wameingia kwenye hii fursa Sukuk" Amesema Muro.
Katika uzinduzi huo Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Fedha BOT, Bw. Sadati Musa amesema Benki kuu kama msimamizi wa sekta ya fedha ina jukumu la kuhakikisha bidhaa na huduma zinazotolewa na mabenki zinafuata taratibu na sheria za nchi.
"Kutolewa kwa hati fungani hii ambayo inaendana na mpango mkuu wa Maendeleo wa sekta ya fedha kama ulivyotolewa na serikali, utawezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kutoa mikopo ya muda wakati kwa sekta za uchumi ikiwemo sekta binafsi na Benki kuu inaamini kuwa mikopo hii itatolewa kwa gharama nafuu" Ameongeza Bw. Sadati.
Fursa Sukuk ni ya miaka mitatu ambayo inafuata misingi ya Shariah kwa kutokutoa riba bali gawio la faida la asilimia 8.75 kwa mwaka.
KCB YAZINDUA HATI FUNGANI YA 'FURSA SUKUK'
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 09, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 09, 2022
Rating:


Post a Comment