NAPE ATAJA SABABU ZILIZOPELEKEA KUSHINDWA KUPELEKA MAPENDEKEZO YA MABADILIKO YA SHERIA BUNGENI
Serikali kupitia Wizara ya habari mawasiliano na teknolojia ya habari imetaja sababu zilizopelekea kushindwa kupeleka mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya habari ambayo wadau wa habari wamekua wakilalamikia baadhi ya katika bunge la Novemba mwaka huu.
Waziri Mwenye dhamana ya kuongoza Wizara hiyo kwa mujibu wa sheria, Nape Nnauye amesema sababu iliyopelekea kushindwa kupeleka mapendekezo hayo bungeni ni kutokamilika kwa baadhi ya taratibu.
Waziri Nape amebainisha hayo alipokuwa akizungumza na uongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Wadau wa Haki ya Kupata Habari (CoRI), jijini Dodoma tarehe 9 Novemba 2022.
" serikali ilitarajia kupeleka mapendekeo hayo lakini haikufanya hivyo kwa kuepuka mivutani kutoka kwa wadau wa habari." amesema Waziri Nape.
‘‘Serikali tupo tayari kupeleka mabadiliko ya sheri ya habari bungeni baada ya kikao cha mwisho. Baada ya kikao hicho tutakubaliana tuliyokubaliana na ndio yataenda,’’ ameongeza Nape.
Amefafanua kuwa serikali haijakaa kimya na bado inaendelea na mchakato huu, huku akibainisha kuwa nia ya serikali bado ni njema
Kwa upande wake Deodatus Balile, Mwenyekiti wa TEF aliomba wadau wa habari kushiriki vema katika kikao cha mwisho cha serikali na wadau wa habari kwa kuwa ni muhimu.
Naye Dk. Rose Reuben, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) alisema, wadau wa habari wanapaswa kutoa mawazo yao ili ifike mahali wakubaliane katika utungaji wa sheria.
NAPE ATAJA SABABU ZILIZOPELEKEA KUSHINDWA KUPELEKA MAPENDEKEZO YA MABADILIKO YA SHERIA BUNGENI
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 09, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 09, 2022
Rating:





Post a Comment