NBAA YAKAGUA MAKAMPUNI 402 YA UKAGUZI, YAADHIMISHA MIAKA 50 TANGU KUANZISHWA KWAKE
Mwenyekiti kamati ya maandalizi ya sherehe za miaka 50 ya NBAA CPA Dr. Neema Kiure akielezea jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius A. Maneno katika ufunguzi wa maonesho ya huduma za kihasibu katika uwanja wa Mnazi Mmoja.
Afisa masoko wa TBS Rhoda Mayugu akimpatia maelezo Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius Maneno mara baada ya kutembelea banda la TBS katika maonesho ya miaka 50 ya NBAA yaliyofunguliwa rasmi leo Alhamisi Novemba 10 katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam
Na Yusuph Digossi - Sauti za Mtaa Blog
Dar es salaam
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius Maneno wakati akifungua maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya NBAA katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam .
CPA Maneno amesema NBAA imeweza kuishauri Serikali katika masuala ya kodi haswa kwenye maboresho na kuongeza wigo wa kodi na kupunguza ambazo zinaharibu jamii .
Ameeleza kuwa NBAA imeweza kukagua makampuni 402 ya ukaguzi na kampuni za simu 102 na kubainisha kuwa idadi ya Wanafunzi imeendelea kuongezeka ambapo kwa sasa kuna wanafunzi takribani 7000.
Amesema shughuli zote za NBAA zinafanyika kwa mfumo wa tehama isipokua shughuli moja ya usimamamizi wa mitihani kutokana na changamoto ya utamaduni wa Tanzania huku akibainisha kuwa changamoto hiyo inafanyiwa kazi.
NBAA YAKAGUA MAKAMPUNI 402 YA UKAGUZI, YAADHIMISHA MIAKA 50 TANGU KUANZISHWA KWAKE
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 11, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 11, 2022
Rating:



Post a Comment