TBS YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA NBAA
Afisa masoko wa TBS Rhoda Mayugu akimpatia maelezo Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius Maneno mara baada ya kutembelea banda la TBS katika maonesho ya miaka 50 ya bodi ya wahasibu Tanzania NBAA yaliyofunguliwa rasmi leo Alhamisi Novemba 10 katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam
Na Yusuph Digossi - Sauti za Mtaa Blog
Dar es salaam
Shirika la Viwango Tanzania TBS limeshiriki maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya wahasibu Tanzania NBAA yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam ambayo yameanza leo alhamisi Novemba 10, 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonesho hayo Afisa masoko wa TBS Rhoda Mayugu amesema kuwa shirika hilo linashiriki maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kuhusu uthibitishaji ubora wa bidhaa .
Amesema TBS inawapa fursa wajasiriamali kudhibitisha bidhaa zao bure kwa muda wa miaka mitatu na baada ya hapo wataanza kulipa aslimia 25 huku akitaja faida atakazopata mjasiriamali baada ya kuthibitisha bidaa yake ni kuuza bidhaa yake ndani na nje ya mipaka ya Tanzania bila kupata kipingamizi chochote.
Pia amesema shirika linawashauri wafanyabiashara wanaoagiza bidaa nje ya nchi wakague bidhaa hizo kabla hazijangizwa nchini ili kuepuka usumbufu ikiwemo kupata hasara baada ya bidhaa yake kukagiliwa hapa nchini na kukutwa na shida.
" Tukikagua bidaa tukaikuta ina shida kwanza tutamwambia arudishe mzigo ulipotoka au ateketeze hapa nchini kwa mujibu wa sheria za NEMC " amesema Rhoda
Pia TBS imekumbusha wafanyabiashara wote wanaofanya biashara inayohusiana na chakula na vipodozi wanaoagiza kutoka nje ya nchi wanatakiwa kusajili bidhaa zao na wenye majengo ya kuhifadhia bidhaa hizo pia wanatakiwa kusajiliwa.
Katika maonesho hayo yaliyofunguliwa rasmi leo Novemba 10 mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius Maneno alitembelea banda la TBS na kupatiwa maelezo ya ushiriki wa TBS katika maonesho hayo.
TBS YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA NBAA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 10, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 10, 2022
Rating:


Post a Comment