WAHITIMU WA MUHAS WANA MCHANGO MKUBWA KATIKA MAENDELEO YA CHUO ' FUN RUN ' YAWAKUTANISHA PAMOJA
Hayo yameelezwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili ( MUHAS ) Prof Appolinary Kamuhabwa wakati wa zoezi la " Muhimbili University Are Union Fun Run " ambalo liliambata na mazoezi ya kukimbia " Marathon" ambalo liliwakutanisha Wanafunzi mbalimbali waliohitimu chuo .
Amesema siku ya Leo ni siku maalumu kwaajili ya wahitimu na washirika wa Chuo cha MUHAS huku akieleza kuwa utaratibu huo umekua ukifanywa na vyuo mbalimbali duniani ambapo wahitimu wamekua wakikutana kwa lengo la kuangalia maendeleo ya Chuo walichosoma na kutoa mawazo yao ili kuhakikisha chuo chao kinaendelea vizuri .
Ameongeza kuwa wahitimu wa chuo cha MUHAS wamekua mchango mkubwa katika kutoa msaada kwa chuo ikiwemo kutoa msaada kwa wanafunzi kufanya mafunzo kwa vitendo kwa ambao wapo kwenye hospitali na sekta mbalimbali Seikalini.
Kwa upande wake mhitimu wa Chuo cha MUHAS ambaye amerudi kufundisha chuoni hapo Dkt. Khadija Malima amesema wameanzisha programu hiyo ili Mwaka 2019 kuwakutanisha wahitimu na kupata mawazo ya kusaidia na kuendeleza Chuo.
" Mwaka huu tukaamua kwamba tunaona magonjwa yasioambukiza kama vile moyo, Kisukari, kiharusi, na unene hivyo tukaona tukutane na kufanya jambo ambalo litagusa jamii nzima wote tumuike kwa kufanya ' Fun Run' . amesema Dktm Malima
Amesema "kutembea hara au kukimbia unasawazisha mapigo ya moyo, mwili inakaa sawa na misuli hivyo tutaifanya hii kama desturi za zoezi hili litakua endelevu"
Aidha Dkt. Malima akatoa wito kwa jamii kushiriki na kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa yasioambukiza ambayo kwa asilimia kubwa husababishwa na kuwa na tabia bwete.
WAHITIMU WA MUHAS WANA MCHANGO MKUBWA KATIKA MAENDELEO YA CHUO ' FUN RUN ' YAWAKUTANISHA PAMOJA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 27, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 27, 2022
Rating:






Post a Comment