Header AD

header ads

Balile alia na madeni ya vyombo vya habari katika taasisi za Serikali



Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),Deidatus Balile, amesema, licha ya kuwepo kwa uhuru wa habari nchini, ameomba uhuru huo ulindwe kisheria.

Akizungumza katika Kongamano la Kwanza la Maendeleo ya Sekta ya Habari leo tarehe 17 Desemba 2022, amesema, wadau wa habari nchini wanafurahia uhuru uliopo lakini haujalindwa kisheria.

“Nimezungumza na Waziri Nape (Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari) kuhusu mjadala wa Sheria ya Huduma za Habari, amesema Januari (2022) mapendekezo yatafikishwa bungeni,” amesema.

Pia Balile amesema madeni ya vyombo vya habari katika serikali na taasisi zake, Balile amesema licha ya juhudi kufanywa, bado taasisi za serikali ikiwemo halmashauri hasijalipa madeni yao kwa vyombo vya habari.
Balile alia na madeni ya vyombo vya habari katika taasisi za Serikali Balile alia na madeni ya vyombo vya habari katika taasisi za Serikali Reviewed by Fahadi Msuya on December 17, 2022 Rating: 5