Header AD

header ads

DCEA yateketeza kilo 2,584.55 za dawa za kulevya




Leo tarehe 21 Disemba, 2022 Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)   kwa kushirikiana na wadau wengine wameteketeza kilo 2,584.55 za dawa za kulevya zinazojumuisha kilo 569.25 za heroin, kilo 15.3 za cocaine na tani mbili za bangi na mirungi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Kamishna Jenerali, Veronica Matikila amesema, uteketezaji huu umefanyika kufuatia kumalizika kwa mashauri ya dawa za kulevya katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, na Mahakama za Hakimu Mkazi za Kisutu na Kibaha Pwani pamoja na Mahakama za Wilaya ya Kinondoni, Ilala, Temeke na Kigamboni.


Dawa za kulevya zilizoteketezwa leo zimehusisha mashauri ya kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2022.


DCEA yateketeza kilo 2,584.55 za dawa za kulevya DCEA yateketeza kilo 2,584.55 za dawa za kulevya Reviewed by Fahadi Msuya on December 21, 2022 Rating: 5