Header AD

header ads

JITIHADA ZA SERIKALI KUTANGAZA FURSA KWA WAWEKEZAJI ZAZAA MATUNDA



Kituo cha Uwekezaji Tanzanzia (TIC)  kimesajili jumla ya miradi 132 sawa na ongezeko la asilimia 22.2 ikilinganishwa na miradi 108 iliyosajiliwa katika kipindi cha mwezi Julai hadi Novemba 2022 mbapo Sekta ya Viwanda imefanikiwa kuongoza kwa kuvutia miradi mingi (67).



Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Desemba 27  jijini Dar es Salaam,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Ndg. John Mathew Mnali Ongezeko hilo kubwa  la Miradi iliyosajiliwa na Kituo cha Uwekezaji linatokana na Jitihada za Serikali za Kutangaza fursa mbalimbali za Uwekezaji zilizoko nchini Tanzania kupitia Ziara mbalimbali za Viongozi wa Kitaifa nje ya nchi pamoja na juhudi za Serikali katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.

Mnali alisema mbali na sekta ya viwanda,  sekta nyingine mbalimbali zilifuata kwa kuvutia miradi mingi ikiwemo Sekta ya Usafirishaji miradi (25), Utalii miradi (12), Kilimo (9), Huduma (8), Majengo ya Biashara (7), Rasilimaliwatu (3) na Sekta ya Fedha (1).

Mnali alisema Miradi hiyo ina jumla ya thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 3.16 na inatarajiwa kutoa ajira 21,297.




JITIHADA ZA SERIKALI KUTANGAZA FURSA KWA WAWEKEZAJI ZAZAA MATUNDA JITIHADA ZA SERIKALI KUTANGAZA FURSA KWA WAWEKEZAJI ZAZAA MATUNDA Reviewed by Fahadi Msuya on December 27, 2022 Rating: 5