Kiwanda cha magari cha GF Vehicles Assemblers (GFA) cha shinda tuzo ya Ubora 2022\2023 kwa makampuni makubwa nchini.
Kiwanda cha kwanza cha kutengeneza na kuunganisha magari nchini Tanzania GF cha Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwan kimeibuka mshindi wa kwanza kwa makampuni makubwa nchini wakati wa utoaji wa tuzo za Ubora wa Kitaifa wa makampuni bora kwa Mwaka 2022\2023 zilizoandaliwa na shirika la viwango nchini TBS.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Kiwanda cha hicho, Ezra Mereng alisema wanaipokea tuzo hiyop kwa furaha kutokana na kushiriki kwa mara ya kwanza na kuibuka kuwa washindi wa jumla katika kipengele cha makampuni makubwa
Pia alisema tuzo hiyo inawahamasisha kuendelea kufanya kazi kwa bidi Zaidi ikiwezekana mwakani washinde tuzo za kimataifa za ubora wa bidhaa na itakayoweza kuzalisha magari na kuingia katika soko la ushindani kimataifa.
Pia aliwashukuru wafanyakazi wenzake wakiongozwa na timu mzima ya wataalamu katika kutengeneza magari vitengo tofauti
Nae mkurugenzi wa shirika la viwango nchini (TBS) ..aliwataka GF kutoridhika na ushindi huo wa jumla nchini na wahakikishe wanashiriki mashindano ya nchi ya SADC katika ubora na viwango kwa makampuni ya jumuia hiyo kuibukja mshindi anapata tiketi ya moja kwa moja ya kushiriki mashindano ya Uboroa na viwango ya jumuia ya SADC na atakuwa anaiwakilisha Tanzania na wao kama TBS watashirikiana na GF kuhakikisha wanapeperusha vyema benderaya Tanzania
Kwa kumalizia mkurugenzi Mtendaji wa GF Vehicles Assemblers (GFA) Imrani Karmal anawapongeza wafanyakazi wake kwa umoja wao ndio chachu ya mafanikio ya wao kukidhi Ubora katika uzalishaji wa magari bila wao wasingweweza kufanikiwa katika ushindi huo.
Kiwanda cha magari cha GF Vehicles Assemblers (GFA) cha shinda tuzo ya Ubora 2022\2023 kwa makampuni makubwa nchini.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 21, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 21, 2022
Rating:



Post a Comment