Header AD

header ads

MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI YANA TIJA KWENYE UHURU WA KUJIELEZA


Na Yusuph Digossi 

Mhadhiri msaidizi kutoka shule kuu ya uandishi habari ya chuo kikuu cha Dar s salaam Mwalimu Elisha Magolanga amesema mabadiliko ya sheria katika vipengele vichache vya sheria ya habari ya mwaka 2016 ambavyo vimekua vikipigiwa kelele na wadau yana tija katika kuongeza uhuru wa watu kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari.


Magolanga ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na Sauti za Mtaa Blog  ambapo alibainisha kuwa sehemu kubwa ambayo wadau wamekua wakipigia kelele ni utaratibu wa kuadhibu vyombo vya habari vinapokesea kufata taratibu za mahakama kama sehemu ya mhimili unaotumika kutoa haki.


Amesema kipengele kinachompa mamlaka Waziri wa habari kuhusika moja kwa moja katika kutoa hukumu kufungia vyombo vya habari sio sahihi na kusema kuwa ni mawazo ambayo yanaweza kujadiliwa, kusikilizwa na kufanyiwa marekebisho.


“ Tuna imani na mhimili wa mahakama katika kufanya kazi na katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeweka wazi hivyo kinachopigiwa kelele na wadau ni sahihi kabisa” amesema
Kuhusu uhuru wa kujieleza na uhuru wa habari una mchango mkubwa katika maendeleo kwasababu Nchi ikiwa na Demokrasia na maendeleo vinakwenda sambamba.


Aidha amepongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kukuza Demokrasia na kushirikiam katika kutanua wigo wa kimataifa hata uhuru wa vyombo vya habari kwasasa unaridhisha.
MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI YANA TIJA KWENYE UHURU WA KUJIELEZA MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI YANA TIJA KWENYE UHURU WA KUJIELEZA Reviewed by Fahadi Msuya on December 02, 2022 Rating: 5