Header AD

header ads

NIC kuendelea kutoa elimu ya Bima ya maisha kwa jamii


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIC, Bw.Lihami Masoli akiwa pamoja na wadau wa NIC wakizindua huduma mpya ya Bima ya BeamLife iliyofanyika Desemba 22,2022 katika Ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam


Na Yusuph Digossi

Shirika la Bima la Taifa NIC limesema kuwa litaendelea kutoa elimu ya kutosha  ya bima ya maisha kwa jamii ili kuhakikisha watu wengi zaidi wanaijua bima ya maisha na kuweza kukata bima hiyo.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam  na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIC, Bw.Lihami Masoli wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya  ya BeamLife yenye lengo la kuwawezesha watanzania katika kujiweka akiba ili kukua kiuchumi kwa mtanzania mmoja mmoja endapo atakata Bima hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIC, Bw.Lihami Masoli akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa huduma ya BeamLife iliyofanyika Desemba 23,2022 katika Ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dar es salaam Bw. Lihami amesema huduma ya bima za maisha za maisha bado haijawafikia watu wengi huku akibainisha kuwa watanzania asilimia 0.3 ndio wenye bima ya maisha hivyo Shirika hilo limeona kuna uhitaji mkubwa wa bima ya maisha hivyo wamezindua huduma hiyo ili kuwafikia watanzania wengi zaidi.

“Kwetu sisi NIC Insurance takwimu hizi ni ishara ya  fursa kubwa ambayotunatakiwa kufikia kwa ubunifu wa bidhaa na utoaji wa huduma bora”. Amesema 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bima za Maisha (NIC) Bw.Hardbet Polepole amesema Bima ya BeamLife imelenga watanzania wote wenye kipato cha juu, cha kati na cha chini
Mkurugenzi wa Bima za Maisha (NIC) Bw.Hardbet Polepole akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa huduma ya BeamLife iliyofanyika Desemba 23,2022 katika Ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakipata picha ya pamoja katika hafla ya Uzinduzi wa huduma ya BeamLife iliyofanyika Desemba 23,2022 katika Ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam.


NIC kuendelea kutoa elimu ya Bima ya maisha kwa jamii NIC kuendelea kutoa elimu ya Bima ya maisha kwa jamii  Reviewed by Fahadi Msuya on December 23, 2022 Rating: 5