Header AD

header ads

Rais Samia Atoa maagizo kwa Wizara 5 Utunzaji wa Mazingira




Na. Beatrice Sanga- MAELEZO

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan ameziagiza Wizara 5 za Kisekta Nchini ikiwemo Kilimo, Uvuvi, Maji Mazingira pamoja na Ufugaji kuketi na kutumia nafasi zitokanazo na Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere huku akisisitiza uhifadhi wa mazingira katika vyanzo vya maji vinavyo jaza Mto Rufiji kutokana na umuhimu wa Mto huo katika Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere.


Rais Samia ametoa maagizo hayo leo  Rufiji Mkoani Pwani wakati wa ufunguzi ujazaji maji katika Bwawa la Mwalimu Nyerere ambapo amesema kwa sasa Sekta zote zenye nafasi ya kuvutia wawekezaji na kutengeneza fursa kutokana na maji ya Bwawa la Mwalimu Nyerere kufanya hivyo ikiwemo Sekta ya Kilimo na Maji ambao ndio watanifaika kupitia Bwawa la Mwalimu Nyerere.



"Nazielekeza Wizara ya Kilimo, Wizara  ya Ardhi na TAMISEMI na mamlaka nyingine mkapime maeneo hayo na muyaweke katika mashamba makubwa kwa ajili ya kufanya mnada wa wazi kwa wawekezaji wa uhakika katika kilimo, nawasihi pia mtenge maeneo maalum kwa ajili ya wakulima wadogowadogo  hasa wa maeneo hayo yatakayokuwa na Miundombinu ya umwagiliaji maji" Amesema Rais Samia


Aidha Rais Dokta Samia ameagiza Wizara ya Mazingira kuchukua hatua dhidi ya waharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji katika mito na maeneo muhimu ambayo yanatumika kama chanzo cha maji katika Bwawa la Mwalimu Nyerere



"Ndugu wananchi manufaa ya Bwawa hili katika nyanja zote yanawezekana tu kama tutatunza mazingira katika vyanzo vya mabonde ya Mito inayoleta maji mabwawani  hapa nataka nisisitize umuhimu wa kutunza mazingira Kwani huu mradi    tumeujenga  kwa gharama kubwa na kwa kujinyima vitu vingi muhimu itakuwa ni dhambi kubwa kama hautatimiza malengo yake kwa sababu ya uzembe na ubinafsi wetu kwahiyo kulinda mazingira na kulinda mradi huu Sasa ni suala la kufa na kupona" Amesema Rais Samia



Kwa upande wake Waziri wa Nishati January Makamba pamoja na Mkurugenzi wa TANESCO maharage Chande wamesema Serikali inaendelea na mipango ya muda ya mrefu ya kukabiliana na changanoto ya umeme ikiwemo kujenga mabwawa manne pamoja na kuanzisha miradi mingine  kupitia  Nishati jadilifu ili kukabiliana na changamoto ya umeme.

 


"Tupo katika kupanga mbele na ukiangalia Ile chati yetu sisi Leo hii tunajua  mpaka 2040 mradi gani utaingia kwenye gridi, tumejipanga kwa muda mrefu na sio kwa muda mfupi, tunachoomba ni subira tatizo la kukatika umeme litaisha, sisi tunataka ndani ya miaka ijayo ibaki historia kwamba  chini ya uongozi wako Mheshimiwa Rais ndipo ulimaliza shida yote ya umeme ya kudumu na Hilo ndilo tunalolifanya  na subira tunayo na  na mipango tunayo hivi Leo tunavozungumza tuna mabwawa mengine mawili ambayo tunatafutia wakandarasi” Amesema Mhe. Makamba


Katika hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi kutoka nchini Misri, Spika wa Bunge Tullia Akson , Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara  Abdulahman Kinana ambapo wakizungumza katika hafla hiyo wameutaja Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kama moja ya Mradi utakao leta mapinduzi katika Sekta ya Nishati  ambayo ni muhimu kwa maendeleo.


Hata hivyo pamoja na zoezi la kubofya kitufe kuashilia kuanza kujaza maji pia Rais Samia amepokea tuzo sanjari na Marais Wastaafu kutokana na kufanikisha ndoto za ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo likikamilika  litazalisha Megawati 2115.
Rais Samia Atoa maagizo kwa Wizara 5 Utunzaji wa Mazingira Rais Samia Atoa maagizo kwa Wizara 5 Utunzaji wa Mazingira Reviewed by Fahadi Msuya on December 23, 2022 Rating: 5