SERIKALI IMEJIPANGA KUKABILIANA NA UGONJWA WA EBOLA ENDAPO UTAINGIA NCHINI
Watoa huduma wa afya zaidi ya 3000 kwa mkoa wa Dar es Salamaa pekee wamepatiwa mafunzo ya namna sahihi ya kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Ebola ikiwa ni tahadhari ambazo Serikali imeanza kuzichukua ili kukabiliana na ugonjwa huo endapo utaingia nchini.
Akizungumza wakati kuwasilisha mafunzo ya namna ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola kwa waandishi wa habari na wazalishaji wa vipindi vya radio na TV mkoani Dar es Salaam, Mratibu wa Kitengo cha Kujikinga na kudhibiti Maambukizi kutoka Wizara ya Afya Dkt. Joseph Hokororo amesema Serikali imejipanga kikamilifu kukabiliana na ugonjwa huo endapo utaingia nchini.
Dkt.Hokororo amesema mbali na mafunzo hayo Serikali kupitia Wizara ya Afya imeandaa pia vifaa kinga vya kuanzia kwa ajili ya watoa huduma watakaohusika moja kwa moja kwenye kuhudumia wagonjwa endapo watajitokeza na pia maeneo ya kuhudumia na kulaza wagonjwa yametengwa tayari.
“tutazidi kuyafikia makundi mbalimbali katika jamii katika kutoa elimu ya namna ya kuzuia na kujikinga na ugonjwa Ebola endapo utajitokeza, watoa huduma za afya tumewafikia, waandishi wa habari tumewafikia na makundi mengine muhimu katika jamii tutahakikisha tunayafkia ili tuweze kushirikiana kwa pamoja katika kutoa elimu ya kuweza kukabiliana na ugonjwa huo endao utaingia nchini kwetu.” Amesema Dkt. Hokororo
Katika Hatua nyingine Dkt. Hokororo amewandoa hofu watanzania kuwa ugonjwa huo kwa sasa bado haujaingia nchini kwetu, hivyo wasiwe na taharuki kikubwa wachukue tahadhari katika kukabiliana na magonjwa yote yanayoambukiza na yasiyoambukiza.
SERIKALI IMEJIPANGA KUKABILIANA NA UGONJWA WA EBOLA ENDAPO UTAINGIA NCHINI
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 13, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 13, 2022
Rating:



Post a Comment