Header AD

header ads

Serikali inatarajia kufanya maboresho katika bandari kuu ya Dar es salaam

DAR ES SALAAM
Serikali inatarajia kufanya maboresho katika bandari kuu ya Dar es salaam ili kuboresha huduma zinazopatikana kupitia bandari hiyo. 

Hayo yamesemwa leo Disemba 1, 2022 na Katibu Mkuu wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Gabriel Migire alipokuwa akizungumza katika mkutano wa Taasisi inayojihusisha na masuala ya usafirishaji wa majini (ISCOS), uliofanyika katika hoteli ya Four Points jijini Dar es salaam.



Migire amesema lengo la Serikali ni kuboresha huduma bora za usafirishaji wa bandari kwa kupitia ushoroba wa bandari ya Dar es Salaam kuzunguka nchi zinazounda umoja huo. Amesema Bandari ya Dar es Salaam ni kiungo kikubwa na cha muhimu katika usafirishaji wa mizigo kwa njia ya maji kwani kwa sasa bandari hiyo inahudumia takribani Asilimia 60% ya mizigo kutoka katika ushoroba huo.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa ISCOS DANIEL KIANGE amesema lengo la mkutano huo ni kujadili juu ya uwasilishwaji wa ripoti inayotaja changamoto zinazoukumba ushoroba wa bandari ya Dar es Salaam ili kuutafutia suluhisho. Pia ametaja baadhi ya changamoto hizo kwamba kuna matumizi ya muda mwingi wa kukagua mizigo mipakani hali inayopelekea ucheleweshwaji wa baadhi ya huduma. 



“kwa uchache tumegundua kwambakuna baadhi ya matatizo hasa hasa upande wa usafiri pale mipakani kunakuwa na wakati mwingi unatumika pale kwa mfano upande wa  Kasumulu hadi Songwe tulitambua kwamba tekinolojia haitumiki sana, kwahivyo unakuta kwamba wakati wanafanya utaratibu wa kuvuka ni njia za kizamani hutumika na hilcho ni kitu ambacho kinachukuwa mud asana. Upande wa Tunduma tulikta kuna skana moja, na ile skana moja haitoshi kwa sababu kuna magari mengi.” Amesema Daniel Kiange 

Intergovernmental Standing Committee on Shipping (ISCOS) ni taasisi inayojihusisha na masuala ya usafirishaji wa majini ambayo kwa sasa inazijumuisha nchi za TANZANIA, KENYA, UGANDA ZAMBIA na DRC. Hivyo basi kikao hicho cha siku mbili kinatarajiwa kutamatishwa hapo kesho huku kikiwa na ufumbuzi wa changamoto zilizoainishwa kwenye ripoti.




Serikali inatarajia kufanya maboresho katika bandari kuu ya Dar es salaam  Serikali inatarajia kufanya maboresho katika bandari kuu ya Dar es salaam Reviewed by Fahadi Msuya on December 01, 2022 Rating: 5