WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA YA MSAMAHA WA MALIMBIKIZO YA KODI YA PANGO LA ARDHI
Serikali kupitia wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi, imetoa rai kwa wananchi wote kutumia kipindi hiki cha siku chache zilizobaki hadi Disemba 31 kunufaika na msamaha wa riba uliotolewa na serikali ya kulipa deni la msingi ili wasamehewe riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Dkt Allan Kijazi wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam ambapo akibainisha kuwa serikali itaanza kuchukua hatua za kisheria kwa watakaokaidi kulipa kodi ya pango la ardhi baada ya kutamatika kwa muda wa msamaha uliotolewa na Rais Dkt. Samia utakapotamatika Desemba 31 mwaka huu.
Dkt. Allan Kijazi amesema idadi ya viwanja ambavyo vimepimwa na wahusika hawajajitokeza kumilikishwa ni 1,457, 809 ambavyo serikali inakusudia kukusanya takribani shilingi 145, 780, 900, 000.
" katika mwaka wa fedha 2022, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa msamaha wa riba ya malimbikizo ya pango la ardhi kwa miezi sita ambayo ilianza kutekelezwa kuanzia Julai 2022 inayoendelea hadi Desemba 2022" amesema
ameongeza kuwa "wananchi walio na malimbikizo wamepewa nafuu ya kulipa deni la msingi ili wasamehewe riba hiyo, watumie nafasi hiyo chache iliyobaki kupata msamaha huo wa riba"
WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA YA MSAMAHA WA MALIMBIKIZO YA KODI YA PANGO LA ARDHI
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 30, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 30, 2022
Rating:

Post a Comment