Header AD

header ads

WANAWAKE WAPEWE NAFASI WALAU ASILIMIA 30 KWENYE VYOMBO VYA HABARI



ILI kukabiliana na rushwa ya ngono pia mfumo dume katika vyumba vya habari, kila chombo cha habari kinapaswa kuwa na dawati la jinsia.

Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari kwenye mkutano uliofanyika tarehe 16 Desemba 2022, jijini Dar es Salaam.

Katika mada iliyochokonolewa na mwendasha mada James Marenga, wakili wa kujitegemea kuhusu wanawake kupewa nafasi walau asilimia 30 kwenye vyombo vya habari, alianza kwa kuhoji sababu za wanawake kuwa wachache kwenye tasnia hiyo.



Kwenye mkutano huo, imeelezwa kwamba miongoni mwa sababu kwa wanawake kupata nafasi za chini katika vyombo vya habari, ni kutojiamini, mfumo dume na rushwa ya ngono.

“Kuna tatizo la rushwa ya ngono kwenye vyumba vya habari, nah ii husababishwa na baadhi ya wanawake kwenye vyumba hivyo vya habari kutojiamini lakini pia mfumo dume,” alisema Lilian Timbuka, mhariri kutoka Gazeti la Mwananchi.

Imeelezwa kwamba, kuanzishwa kwa madawati ya jinsia katika vyumba vya habari kutatoa fursa kwa wale watakaofanyiwa matukio kinyume na maadili ya tasnia hiyo, kuwa na mahali pa kupata msaada.

Akichangia mada hiyo, Deodatus Balile ambaye ni Mwenyekiti wa TEF, alisema miongoni mwa sababu kwa wanawake kuangukia kwenye rushwa ya ngono kwenye vyumba vya habari ni kutokana na ugeni.

“Wapo wanaoangukia kwenye rushwa ya ngono kwa sababu wanawahiwa kwa kuwa ni wageni, ugeni huo unaambatana na woga.



WANAWAKE WAPEWE NAFASI WALAU ASILIMIA 30 KWENYE VYOMBO VYA HABARI WANAWAKE WAPEWE NAFASI WALAU ASILIMIA 30 KWENYE VYOMBO VYA HABARI Reviewed by Fahadi Msuya on December 17, 2022 Rating: 5