Header AD

header ads

DEMOKRASIA INALETA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI



Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini amesema, vyombo vya habari vikiwa huru, malengo ya kuanzishwa kwake yatafikiwa.

Ametoa kauli hiyo akizungumza na baadhi ya waandishi leo tarehe 16 Januari 2023, jijini Dar es Salaam.

Amesema kukiwa na Demokrasia basi vyombo vya habari vitakua huru kwasababu sheria zitakua nzuri sio za ukandamizaji hivyo watu watakua huru kutoa mawazo na kukosoa 

Pia ametaja mambo mbalimbali ambayo yatasaidia nchi ikiwa vyombo vya habari nchini vitakuwa huru.

Amesema  Serikali ina nafasi nzuri ya kuweza kujitathmini katika utendaji wao ja kuangalia kama wanakwenda vizuri au hawaendi sawa sawa.

"Vyombo vya habari ni kama kioo kwa serikali na sekta binafsi, hivyo vikiwa huru vitaweza kusaidia serikali kufanya tathmini ya utendaji kazi wake" - Sheikh Ponda

DEMOKRASIA INALETA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI DEMOKRASIA INALETA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI Reviewed by Fahadi Msuya on January 16, 2023 Rating: 5